Slider

BILIONI 8 KUPANUA UWANJA WA NDEGE MWANZA
Local News

UJENZI kwa ajili ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza unaendelea kwa kasi baada ya serikali kulipa kiasi cha fedha kwa mkandarasi. Imeelezwa kuwa Serikali imeshatoa Shilingi Bilioni Nne kwa Mkandarasi ambaye ni Kampuni ya BCEG ya China. Ukarabati unaofanywa ni upanuzi wa Uwanja wa kuongeza njia za kurukia ndege, jengo la kuongozea ndege na ghala la mizigo. Kiasi hicho cha fedha kinafanya fedha ambazo serikali imeshamilipa Mkandarasi kufikia Shilingi Bilioni 13. Meneja wa Uwanja huo ESTHER MADALE amesema...

Like
442
0
Thursday, 20 November 2014
MAHIZA: WIKI MOJA TU LA SIVYO!!!
Local News

  MKUU WA MKOA wa Pwani Mwantumu Mahiza ametoa muda wa Wiki moja kwa watendaji wa Wizara ya Ardhi na Wizara ya Maliasili na Utalii kulipatia ufumbuzi suala la uvamizi wa Hifadhi ya Kazimzumbwi. MAHIZA ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya kutembelea Hifadhi hiyo ambapo alifuatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo. Amebainisha kuwa hifadhi hiyo ipo hatarini kutoweka na kuvamiwa na watu walioweka makazi ya kudumu na kuendesha shughuli mbalimbali....

Like
1095
0
Thursday, 20 November 2014
ANGELINA JOLIE KUACHA KUFANYA FILAMU!!!
Entertanment

Angelina Jolie kwa sasa anafilamu mbili anazozifanyia kazi Unbroken na By the Sea .Muigizaji huyo wa Hollywood kwa sasa ndie nyota wa majarida mawili Variety na DuJour Katika mahojiano yake na jarida la DuJour Angelina alizungumzia jinsi anavyofanyakazi na mumewe Brad pitt kwenye scene tofauti Kuhusu swala la kuacha kuigiza Angelina alisema “Sikuwahi kupenda kuwa mbele ya Camera wala sijawahi kufikiria kuongoza filam ila natumai kuwa na fani hii kwa sababu ninaifurahia saana”  pia alizungumzia jinsi anavyofanya filam ya By...

Like
334
0
Thursday, 20 November 2014
EBOLA: MFUKO WA BILL NA MELINDA GATES UMEAHIDI KUTOA DOLA MILONI 5.7
Global News

MFUKO wa Bill na Melinda Gates umeahidi kutoa kiasi cha dola milioni 5.7 kwa ajili ya mradi kusaidia matibabu dhidi ya maradhi ya Ebola nchini Guinea na nchi nyingine zilizoathiriwa na ugonjwa huo. Mfuko huo pia umesema msaada huo utasaidia kutathimini dawa za majaribio. Zaidi ya Watu 5,000 wamepoteza maisha kutokana na Ebola, karibu wote kutoka Afrika Magharibi. Hata hivyo kuna chanjo kadhaa za majaribio na dawa za kutibu maradhi ya Ebola, lakini hazijajaribiwa kwa ajili ya kuona usalama wake...

Like
336
0
Wednesday, 19 November 2014
CAF YATISHIA KUTOFANYIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
Local News

CHAMA cha Wananchi -CUF kimetishia kutofanyika kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa endapo Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI haitabadilisha utaratibu waliouweka wa upigaji kura. Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Naibu Katibu Mkuu Bara Magdalena Sakaya amesema kuwa chama hicho hakitakubali kuona wagombea wao wanaenguliwa kulingana na mwongozo na kanuni za uchaguzi zilizopo ambazo tayari waliitaka TAMISEMI kuzirekebisha kwani zina mapungufu kwa wagombea na hata wapiga kura....

Like
351
0
Wednesday, 19 November 2014
MILIONI 568 ZATUMIKA KUJENGA VYUMBA VYA MAABARA KATIKA SHULE 17 MPANDA
Local News

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imefanikiwa kujenga vyumba 17 vya maabara kwa shule zake sita za Sekondari kwa gharama ya shilingi 568.6 milioni. Hatua ya ujenzi wa maabara hizo umekuja ikiwa ni sehemu ya kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu ujenzi wa vyumba vya Maabara kwa Shule za Sekondari nchini. Akiwasilisha  taarifa ya utekelezaji wa  ujenzi wa maabara kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima aliyekuwa Mwenyekiti wa  Kikao...

Like
394
0
Wednesday, 19 November 2014
TUTAPAMBANA YAPOKEA MILIONI 5 KUENDELEZA KIKUNDI HICHO
Local News

JUMLA ya shilingi milioni tano zimetolewa na Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Abdul Azizi Mohamed Abood katika kikundi cha kuweka na kukopa cha Tutapambana Silk kilichopo Chamwino Mjini Morogoro kwa ajili ya kuendeleza kikundi hicho katika miradi mbalimbali ya maendeleo. Akipokea msaada huo Katibu wa kikundi hicho Omary Simbeye amesema kuwa fedha hizo zitawasaidia kuweza kuiendeleza miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kujenga ofisi na kukabiliana na changamoto mbalimbali za ukosefu wa ofisi katika kikundi hicho. Aidha amesema...

Like
298
0
Wednesday, 19 November 2014
CHRIS BROWN APIGA GRAFFITI YA MASHAHIRI YA 2PAC KWENYE LAMBORGHINI YAKE
Entertanment

Huenda Chris Brown anamapenzi yakupitiliza juu Graffiti hadi kufikia kuichora gari yake graffiti ya mashahiri ya 2pac lenye thamani ya dola za kimarekani $750,000. Chris Brown alishea picha za gari hilo lenye rangi nyeusi kupitia akaunti yake ya...

Like
1438
0
Wednesday, 19 November 2014
JIBU LA VANESSA MDEE KUHUSU MAHUSIANO YAKE NA JUX
Entertanment

Jibu la Vanessa Mdee kuhusu mahusiano yake na Jux ni kwamba “Tunapendana” Mapema leo kupitia kipindi Cha Genge ndani ya 93.7efm . Bagdad alimuuliza vanesa Mdee juu ya taarifa zilizokuwa zikivuma kwamba yupo kwenye Mahusiano na Jux Vanessa alijibu “TUNAPENDANA” Lakini wakizungumzia kuhusu kufanya wimbo mwingine wa pamoja kati ya Vanessa na Barnaba wamesema kwamba mashabiki wao wasubiri huenda kuna kitu kikafuata mara baada ya project ya Siri....

Like
913
0
Wednesday, 19 November 2014
UN: KOREA KASKAZINI INASTAHILI KUFIKISHWA KWENYE MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA UHALIFU
Global News

BARAZA la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu limesema Korea Kaskazini inastahili kufikishwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu kutokana na kukiuka haki za binadamu. Katika baraza hilo zimetolewa tuhuma dhidi ya Korea Kaskazini kwamba serikali yake imekuwa ikifanya vitendo vya ukiukaji haki za binadamu. Mapendekezo hayo yaliyopitishwa na baraza la haki za binadamu la kimataifa yanapaswa kupigiwa kura ili kupitishwa na bunge yaweze kuhalalishwa. Ripoti ya mwezi Februari mwaka huu iliyotolewa na umoja wa mataifa ilibainisha kuwa watu...

Like
290
0
Wednesday, 19 November 2014
MAREKANI YAIPONGEZA BURKINA FASO
Global News

SERIKALI ya Marekani imewapongeza wananchi wa Burkina Faso na viongozi wao kwa kutia saini mkataba utakao ongoza serikali ya mpito kuelekea serikali iliyochaguliwa kidemokrasia. Aidha Marekani imesema inampongeza Michel Kafando kwa kuapishwa kuwa rais wa mpito wa Burkina Faso na kuendeleza kasi iliyoanza wiki mbili zilizopita na kuwachagua watu watakaosaidia kuendesha serikali ya mpito ambao wamejitolea kujenga serikali ya kiraia na kidemokrasia. Hata hivyo imeyataka majeshi ya Burkina Faso kuendelea na jukumu lao la msingi la kulinda mipaka...

Like
355
0
Wednesday, 19 November 2014