WAFANYABIASHARA wa soko la Buguruni wameiomba Serikali kuwasaidia kuwajengea miundombinu ya soko hilo ili kuwasaidia kupunguza hasara ya uharibifu wa biashara zao. Wakizungumza na Efm leo, wafanyabiashara hao wamesema wamekuwa wakipata hasara kubwa hususani upande wa biashara ya Matunda kwakuwa huoza kutokana na kutokuwepo kwa mifereji ya kupitishia maji kipindi cha msimu wa Mvua. ...
JESHI la Burkina Faso limeapa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa baada ya kuimarisha udhibiti wake katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi. Vikosi vya usalama hapo jana vimefyatua mabomu ya kutoa machozi na risasi angani ili kuwatawanya waandamanaji wanaopinga hatua ya jeshi kutwaa madaraka baada ya Rais Blaise Compaore kujiuzulu. Majeshi yaliingia katika uwanja maarufu wa Place de la Nation mjini Ouagadougou na kuchukua udhibiti wa makao makuu ya televisheni ya taifa katika hatua ya kuonyesha ubabe, licha ya wito...
WATU 60 wameuawa katika shambulizi la bomu la kujitoa mhanga nchini Pakistan karibu na mpaka na India, ikiwa ni shambulizi baya zaidi la kigaidi kuwahi kutokea nchini humo katika miaka ya hivi karibuni. Makundi kadhaa, likiwemo la Taliban, yamedai kuhusika na shambulizi hilo ambalo liliwajeruhi zaidi ya watu 120, lililotokea karibu na kivuko pekee cha mpaka kati ya Pakistan na India cha Wagah mashariki ya mji wa mashariki mwa Pakistan, Lahore. Shambulizi hilo lilitokea baada ya kukamilika sherehe maalumu za kijeshi...
Msanii kutoka Nigeria anaefanya vizuri kwa sasa kwenye tasnia ya muziki kwa sasa Iyanya maarufu kama Mr. Kukere jina lililotoka kwenye wimbo wake. hivi karibuni timu nzima ya Triple MG record label na wasanii wke akiwemo Iyanya wapo nchini Uingereza kwenye tour maalum ya kimuziki ambapo wasanii na mashabiki kwa pamoja walijumuika kusherehekea siku ya kuzaliwa ya msanii huyo, wengine ambao walikuwepo kwenye eneo hilo ni pamoja na mwimbaji Emma Nyra pamoja na meneja wa Iyanya Ubi Franklin. tazaama baadhi ya picha...
Msanii kutoka marekani mzaliwa wa Saint Michael, huko Barbados, mwaka 1988 February 20, alifungiwa kuendelea kutumia mtandao wa instagram kwa takribani miezi sita mara baada ya kukiuka taratibu za mtandao huo. miezi michache nyuma msanii huyo alipost picha yake kwenye akaunti ya Instagram akiwa hana top kuziba mwili wake sehem ya juu hivyo kumfanya kuwa mtupu picha alizopiga kwenye photoshoot ya jarida la Lui. picha hiyo iliondolewa haraka na uongozi wa mtandao huo na akaunti yake ilifutwa kabisa baada ya muda mfupi...
Baada ya kuonyesha mjengo wake alioupa hadhi ya nyota Tano miezi kadhaa nyuma sasa msanii kutoka Nigeria ambae ametambulika zaidi kwenye ramani ya muziki wa Afrika baada ya Kuachia ngoma yake iliyopewa jina maarufu kama Limpopo K cee ameshea picha za gari lake jipya aina ya Cadillac Escalade 2014 yenye bodi iliyopambwa na dhahabu K cee alishea picha hizo kupitia Akaunti yake ya Instagram ambapo aliandika Caption ya maneno haya “So far this year God has been so good to...
French Montana alizaliwa huko Karim Kharbouch mwaka 1984 ndani ya Rabat, Morocco, rapa huyo wa kimarekani ni mwanzilishi na mmiliki wa Cocaine City Records , lakini mwaka 2012 alisaini mkataba na kampuni za Maybach Music Group and Bad Boy Records, umaarufu wake umekuja zaidi kufuatia kolabo zake na wasanii tofauti ikiwemo Max B, rick rose n.k Kupitia interview aliyoifanya kwenye kipindi cha Sway in the Morning rapa huyo ametangaza kuachia albamu yake ya Mac & Chees hapo December 16 baada...
Winga wa klabu ya Celtic, Aleksandar Tonev amepewa adhabu ya kutokucheza mechi nne baada ya kukutwa na hatia ya kitendo cha ubaguzi wa rangi. Raia huyo wa Bulgaria mwenye umri wa miaka 24 alifanya kitendo hicho kwa beki wa klabu ya Aberdeen, Shay Logan mwezi tisa mwaka huu mchezo ambao Celtic waliibuka na ushindi wa goli 2-1. Uongozi wa klabu ya Celtic umesema adhabu hiyo ni kali na hawaamini kama...
Klabu ya Manchester United imefikia makubaliano na klabu ya AS Monaco juu ya ada ya kumsajili moja kwa moja mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao. Falcao alijiunga na klabu ya Manchester United kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea AS Monaco kwa dau la euro million 8 huku kukiwa na kipengele kinachomruhusu kujiunga na mashetani wekundu mwisho wa mkataba huo. Manchester United chini ya Ed-Woodward wamesema wapo teyari kulipa kiasi cha euro million 56 na mshahara wa kiasi cha...
IMEELEZWA kuwa idadi kubwa ya vijana wasiokuwa na ajira nchini wako hatarini kuingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya kufuatia ongezeko kubwa la uingizaji wa dawa hizo nchini Akizungumza na E fm Mkurugenzi wa Maa media FURAHA LEVILAL amefafanua namna mradi huo utakavyoweza kukomboa fikra za vijana ili kuongeza uchumi wa taifa… FURAHA LEVILAL Naye kaimu mkuu wa masoko na uhusiano wa NBC RUKIA MKINGWA ameeleza kuwa vijana ni nguvu kazi ya taifa hivyo wajitokeze kwa wingi kushiriki fursa hiyo.………RUKIA...
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa LAZARO NYALANDU amezindua rasmi Mkakati wa Taifa wa Kupambana na Ujangili dhidi ya Wanyama pori na bihashara haramu ya meno ya Tembo nchini. Akizungamza na wadau mbalimbali Jijini Dar es Salaam NYALANDU amesema kuwa Mamlaka ya Wanyama Pori imepewa jukumu la kusimamia shughuli zote za uhifadhi wanyama kwa asilimia 90 sawa na kilomita za mraba laki moja na elfu sabini. NYALANDU ...