Baada ya Meneja wa Diamond kushikiliwa na polisi kwa ajiri ya kufanyiwa mahojiano kuhusiana na swala la msanii huyo kutumia sare za jeshi kwenye tamsha wakati anafanya Show, Leo inasemekana pia Diamond anashikiliwa na polisi leo kwa mahojiano zaidi kufuatia tukio hilo katika kituo cha Oysterbay Bagdad amezungumza na msemaji wa jeshi ili kujua taratibu zitakazofuatwa kulingana na kosa husika, Hata hivyo msemaji huyo ameongeza ya kuwa sheria itachukua mkondo wake ...
Katika ligi ya mabingwa barani Ulaya Liverpool imechabangwa nyumbani Anfield kwa mabao 3-0 kutoka kwa Real Madrid huku Mario Balotelli akiingia lawamani. Meneja wa mchezaji huyo mtukutu, Brendan Rodgers amemlaumu mshambuliaji huyo kwa kitendo chake cha kubadilishana Jezi na Pepe mara tu baada ya dakika 45 za kwanza. Baadhi ya mashabiki wa jijini Dar es Salaam,Tanzania wamemtupia lawama mchezaji huyo ambaye pamoja na kununuliwa kwa pauni milioni 16 ameifungia Liverpool goli moja tu msimu huu. Wakati huo huo Arsenal wamepata...
WATANZANIA wameshauriwa kutotegemea zaidi ugunduzi wa mafuta na gesi kuwa ndio njia pekee ya kutatua matatizo ya kiuchumi nchini. Akizungumza na wadau mbalimbali jijini Dar es salaam kwenye kongamano la kufunga maonesho ya tatu ya mafuta na gesi asilia Naibu Waziri wa Nishati na Madini mheshimiwa STEVEN MASELE amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutumia fursa hiyo kama njia moja wapo ya kuinua vyanzo vingine vya uchumi MASELE Aidha Mheshimiwa MASELE amebainisha kuwa Serikali imeandaa mkakati wa kufungua mfuko utakaotumika kuifadhi mapato...
KAMATI ya Hesabu za Serikali za mitaa inatarajia kwenda kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kukagua mapato na matumizi katika Halmashauri za mikoa ya Mwanza na Iringa. Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa Kamati hiyo RAJAB MBARUK MOHAMED ambapo amesema Kamati itaondoka leo kwa kuwa ripoti ya CAG inaonyesha kuwa Mwanza ndiyo ilifanya vibaya zaidi kuliko zote…. Hata hivyo amesema, kuna fedha zaidi ya bilioni mia tatu zilizotolewa na wafadhiri kwa ajili ya Halmashauri hazikutumika. MOHAMED...
Ikiwa ni siku kadhaa toka stori za Nicki Minaj na Safaree Samuels mahusiano yao kuyumba, hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii kufuatia post zilizotumwa na wawili hao katika muda tofauti huku kila mmoja akiandika maneno yake mahusiano ya wawili hawa yaliyodumu kwa miaka isyopungua kumi na nne (14) kwa sasa hayapo tena, na hii imekuja mara baada ya Safaree Samuels kuonekana amezificha tatoo za Nicki minaj kwenye mwili wake kwa kuchora tatoo nyinginge mpya kwa juu yake kama alivyowahi kufanya Nick...
Mchezaji wa QPR Adel Taarabt amemjibu kocha wake Harry Redknapp aliyesema kuwa mchezaji huyo ana uzani mkubwa hivyobasi hafai kucheza. Redknapp alitoa madai hayo alipoulizwa ni kwa nini hakumjumuisha kiungo huyo wa kati katika kikosi kilichocheza mechi dhidi ya Liverpool waliposhindwa kwa mabao 3-2. Hata hivyo Taarabt alipokuwa akiongea na kituo cha habari cha Daily Mail alijitetea kwamba madai hayo si ya kweli. “Nilikuwa na tamaa kubwa ya kucheza kabla ya mechi kuanza. Nilikasirika sana niliponyimwa nafasi ya kucheza.”alisema...
Wachezaji wa Sunderland wameamua kuwarudishia Mashabiki wao gharama walizotumia kuutizama mchezo ambao mwisho wa siku walipokea kichapo cha bao 8-0 kutoka kwa Southampton. Hicho kilikuwa kisago kikubwa kabisa kwa Sunderland katika miaka 32. Mashabiki wana nafasi ya kudai pesa yao mpaka kufikia tarehe 5 ya Novemba mwaka huu. Akizungumza kwa niaba ya wenzake, nahodha John O’Shea amesema, “Tunashinda na kushindwa kama timu, wachezaji, uongozi na mashabiki lakini tungependa kuwatambua na kuwashukuru mashabiki waliosafiri umbali mrefu kuja...
kufuatia tuhuma mbalimbali juu ya mshindi wa shindano la Miss Tanzania kwamba hakustahili kupata taji hilo na kuwepo kwa taarifa zenye kuchanganya kuhusu umri wa mlimbwende huyo Sitti Mtemvu, jana kamati ya Miss Tanzania ilifanya kikao ikiwa pamoja na kujadili na waandishi wa habari ili kuweka mambo sawa kwa kutoa vielelezo vyao. hata hivyo hali ya Sintofahamu bado imeendelea kuwepo kwenye baadhi ya vichwa vya watu kupitia mitandao ya kijamii na sehemu nyinginezo kufuatia baadhi ya majibu ya Mrembo huyo wakati akihojiwa...
SHIRIKA la umeme nchini Tanesco kwa kushirikiana na wakala wa umeme vijijini -REA- wamefanikiwa kupeleka wataalamu wakutoa elimu ya matumizi sahihi na salama ya umeme katika vijiji vyote vya wilaya ya mkuranga ikiwa ni utekelezaji wa ahadi waliyoitoa kupitia kwa naibu waziri wa fedha ADAMU MALIMA. Akizungumza na EFM Ofisini kwake jijini Dar es salaam meneja wa Tanesco kanda ya Pwani na Dar es salaam MAHENDE MUGAYA amesema kuwa wataalamu hao watatoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutumia...
BARAZA la habari nchini-MCT kwakushirikiana na Kamati ya maandalizi ya tuzo za Umahiri za uandishi wa habari Tanzania-EJAT, leo imezindua rasmi tuzo hizo ikiwa ni mara ya sita tangu kuanzishwa kwake. Akizungumza na wandishi wa habari Jijini Dar es salaam, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya EJAT, Meneja udhibiti na viwango wa MCT, Pili Mtambalike amesema tuzo za mwaka huu zimeongezewa mambo mapya mawili nakufanya jumla ya makundi ya kushindaniwa kuwa 21 kutoka 19. PICHA NI BAADHI...
VIKAO vya kamati za Bunge vimeendelea leo jijini Dar es salaam ikiwa ni siku ya pili ambapo ripoti za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma zimewasilishwa zikifatiwa na taarifa ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2012-2013 Katika Kamati ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma-PAC. Akisoma Ripoti ya CAG, mbele ya mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe, Msaidizi Mkaguzi Mkuu Nestory Karia amesema ofisi yake imebaini mapungufu mengi ya fedha katika baadhi...