Marekani imesitisha sera ya muda mrefu ambayo ilikuwa inawapa raia wa Cuba hadhi maalumu ya kuingia na kuishi nchini Marekani bila ya visa. Serikali ya Cuba imekuwa ikilalamika kwamba, sera hiyo, ijulikanayo kama “wet foot, dry foot,” imewafanya maelfu ya raia wa Cuba kukimbia nchini humo kila mwaka. Rais Obama amesema hatua ya kuondolewa kwa sera hiyo, ni hatua muhimu katika kurudisha uhusiano na Cuba. Mahasimu hao wa muda mrefu wamerudisha uhusiano wa kidiplomasia mnamo mwaka 2015 baada ya karne...
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, amesema mitandao ya idara za ulinzi za nchi zilishambuliwa mara 24,000 mwaka jana peke yake lakini udukuzi huo ulizimwa. Jean Yves-Le Drian, alisema udukuzi kama huo unaongezeka mara dufu kila mwaka. Alionya kuwa miundo mbinu ya taifa iko kwenye hatari, na kwamba kunaweza kufanywa jaribio la kuchafua uchaguzi wa mwaka huu. Bwana Le Drian amekuwa akisimamia mabadiliko makubwa katika mifumo ya mitandao ya Ufaransa, ambapo mkuu wa jeshi ataongoza operesheni mpya za komputa, Cybercom. Waziri...
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Boris Johnson amekutana na washauri wakuu wa rais mteule wa Marekani Donald Trump mjini New York, Marekani. Johnson alikuwa na shemejiye Trump, Jared Kuchner, na afisa mkuu wa mikakati wa Bw Trump Steve Bannon. Huo ulikuwa mkutano wa kwanza wa ana kwa ana kati ya maafisa wa Trump na waziri wa Uingereza. Maafisa wanasema kwenye mkutano huo, sera ya Marekani kuhusu Syria, China na Urusi ilijadiliwa. Jumatatu, Bw Johnson atakuwa mjini Washington D.C,...
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemshinda mpinzani wake Lionel Messi na kupata tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or hii ikiwa ni kwa mara ya nne. Ronaldo mwenye miaka 31 sasa anahitaji tuzo moja tu kumfikia Messi ambaye mwaka jana alipata tuzo ya tano. Mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann amemaliza katika nafasi ya tatu. Ronaldo aliisaidia Madrid kushinda ligi ya mabingwa ulaya msimu uliopita sambamba na kuisaidia nchi yake ya Ureno...
Mpango wa uuzwaji wa klabu ya Ac Milan wasogezawa mbele hadi mwakani mwezi wa tatu. Klabu hiyo ya nchini Italy inayomilikiwa na aliyewahi kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Bwana Silvio Berlusconi ilitajwa kuuzwa kwa wawekezaji wa China mwezi huu wa kumi na mbili lakini mpango huo umesogezwa mbele hadi mwakani mwezi wa...
Waamuzi waliochezesha mchezo namba 49 kati ya Yanga na Simba, Martin Saanya na Samweli Mpenzu wametolewa kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, huku suala lao likipelekwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili ishughulikie tatizo lao kitaalam. Maamuzi hayo yamefanyika baada ya Kikao cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya Bodi ya ligi, kuwaita na kuwahoji na kuangalia mkanda wa mchezo husika. Kamati imebaini mapungufu mengi ya kiutendaji yaliyofanywa na waamuzi hao, na hivyo kuitaka kamati ya waamuzi ishughulikie....
Kiongozi wa Sudan Omar el Bashir amempongeza rais mteule wa Marekani Donald Trump akisema kuwa itakuwa rahisi kushirikiana naye, kulingana na gazeti la Emirati al Khaljee. ”Bw Trump anaangazia maslahi ya raia wa Marekani, ikilinganishwa na wale wanaozungumzia kuhusu demokrasia ,haki za kibinaadamu na uwazi”,alisema rais Bashir katika mahojiano na gazeti hilo. Aliongezea kwamba: Tunaweza kushirikina na watu wenye sura mbili lakini huyu hapa mtu mwenye uwazi wa anajua anacholenga. ”Nina hakika itakuwa rais kushirikiana na Trump...
Kibaha. Jeshi la Polisi mkoani Pwani limezungumzia kifo cha askari wake PC Armand Furaha (33) aliyejipiga risasi kifuani bila kukusudia na kufariki dunia. Askari huyo alijipiga risasi hiyo usiku akiwa anaelekea kwenye lindo nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha. Tulio hilo lilitokea saa moja usiku eneo la Mailimoja sokoni usiku wa kuamkia jana, wakati askari huyo akiwa njiani kuelekea kwenye kituo cha lindo alichopangiwa. Kaimu Kamanda wa Polisi Pwani, Blasius Chatanda amesema askari huyo alijipiga risasi bahati mbaya kwa...
Rais mteule wa Marekani Donald Trump anajiandaa kutangaza mawaziri zaidi watakaohudumia utawala wake. Ripoti zinasema kwamba Trump atamteua mshirika wake wa kibiashara wa zamani Steven Mnuchin kama waziri wa fedha. Wawili hao walikuwa wanamiliki Goldman Sachs, kampuni ambayo Trump aliikashifu wakati wa kampeni zake. Pia ameshiriki mazungumzo na Mitt Romney, ambaye anakisiwa kuwa mwaniaji wa wadhfa wa waziri wa mambo ya kigeni. Bwana Romney aliyewania urais kwa tiketi ya chama cha Republican mwaka 2012, kwa wakati mmoja alimwita Trump mtu...
Uongozi wa klabu ya Simba umesema kwamba kwa sasa hawatacheza mechi yeyote ile dhidi ya Yanga endapo TFF itaendelea kupanga waamuzi wa hapa nyumbani. Mkuu wa mawasiliano wa Simba Haji Manara amesema kuwa kama wao viongozi wameamua kufanya hivyo kwani waamuzi wa hapa nyumbani wamekuwa hawatendi haki kwa upande wao kwani mara nyingi hutoa maamuzi tofauti juu yao. “Angalia mechi yetu dhidi ya Yanga,Martine Saanya anakataa goli halali la Ibrahimu Hajibu baadae anakubali goli la mkono lililofungwa na Amisi Tambwe,mwamuzi...
Mchungani wa Afrika kusini ambaye aliwapulizia dawa ya kuua wadudu inayoitwa Doom waumini amelaaniwa vikali. Katika taarifa aliyoituma kwenye ukurasa wa Facebook, pmchungaji aliyejitangaza kama nabii Lethebo Rabalago alidai dawa ya kuua waduduinayojulikana kama Doom inaweza kuwaponya wengi. Kampuni inayozalisha Doom imeonya juu ya hatari ya kupuliza dawa hiyo watu , huku tume maalum ya serikali ikimtaka yoyote atayeathirika kuwasilisha malalamiko. Lakini mchungaji huyo ametetea kitendo hicho, akiiambia BBC kuwa anatumia mbinu zisizo za kawaida...