SHIRIKA la Umeme Nchini (Tanesco) limetakiwa kuandaa mpango madhubuti wa utitirishaji maji kutoka kwenye bwawa la Nyumba ya Mungu ili kuwepo na maji ya kutosha kuzalisha umeme kwenye vituo vya Hale na New Pangani. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake katika mabwawa ya kuzalishia umeme ya Hale na Pangani yaliyoko mkoani Tanga na bwawa la Nyumba ya Mungu la mkoani Kilimanjaro. Agizo hilo alilitoa baada ya kujionea namna ambavyo...
MAKAMU wa Rais Mheshimiwa mama Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo linakwenda sambamba na Shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 kwa amani na utulivu, uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la KKKT, Dokta Alex Malasusa amesema ni jambo jema kumshukuru Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani na utulivu...
Na. Omary Katanga………………………………..+255784500028 Kila unapofika wakati wa usajili kwa wachezaji kutoka klabu moja kwenda kujiunga na klabu nyingine,malalamiko,vitisho,ubabe na hata kutunishiana misuli kwa baadhi ya viongozi wa klabu kwa kile kinachoonekana wengine kufuata kanuni na wengine kuzitupilia mbali. Tofauti na Tanzania,kwa upande wa nchi nyingine zilizoendelea kisoka duniani huwezi kusikia malalamiko kama hayo yaliyopo hapa nchini kuhusu usajili,na hii ni kutokana na utaratibu mzuri uliokuwepo kati ya...
Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya Uefa Michel Platini ameshindwa katika rufaa yake ya kutaka marufuku ya siku 90 dhidi yake iondolewe. Alikuwa amewasilisha rufaa akitaka marufuku ya kutojihusisha na soka kwa miezi mitatu iondolewe kumuwezesha kuendelea na kazi lakini hilo limekataliwa na Mahakama ya Mizozo ya Michezo. Platini, 60, alisimamishwa kazi pamoja na rais wa Fifa Sepp Blatter mwezi Oktoba huku uchunguzi wa madai ya rushwa dhidi yao yakiendelea kuchunguzwa. Wote wawili wamekanusha tuhuma...
RAIS Xi Jinping wa China na Barack Obama wa Marekani walikuwa na mazungumzo ya simu leo na kuahidi kwamba nchi zao zitaendelea kushirikiana katika suala la mabadiliko ya tabia nchi. Televisheni ya taifa nchini China imeripoti kwamba marais hao wawili wamesema watashirikiana kwa karibu kuendeleza mafanikio yatakayotokana na mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tabia nchi unaoendelea mjini Paris, Nchini Ufaransa....
TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini-NEC-imewataka Wananchi waliojiandikisha kupiga Kura katika Majimbo na Kata husika, kujitokeza kwenye vituo walikojiandikisha siku ya Jumapili ili kuweza kupiga Kura na kuwachagua viongozi wanaowataka. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Damiani Lubuva amesisitiza kwamba taratibu zilizotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu ndizo zitakazotumika katika uchaguzi...
KUFUATIA kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya Nguruwe MKoani Mwanza, wafugaji wametakiwa kuepuka kununua Nguruwe kutoka kwenye Maeneo au Mashamba yenye ugonjwa Nguruwe na kutakiwa wafugwe kwenye Mabanda imara ili waepuke kutembea ovyo , Nguruwe wasilishwe mizoga au masalio ya chakula kutoka vyanzo visivyojulikana . Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Dokta Yohana Sagenge , Mlipuko huo umedhibitishwa kutokana na uchunguzi uliofanyawa na Maabara ya Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) nakubainishwa...
IKIWA imepita siku moja tokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli atangaze Baraza jipya la Mawaziri lenye Wizara 19, Mawaziri 18 huku Wizara nne zikiwa bado hazina Mawaziri baadhi ya Wananchi wakiwemo wasomi na Wafanyabiashara wamekuwa na maoni mbalimbali huku wengi wakilipongeza. Akizungumza na Efm jijini Dar es salaam Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dokta Benson Bana amesema kuwa uteuzi uliofanywa ni uteuzi ambao haujangalia uso na majina ya Viongozi bali...
SHIRIKA la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema jana kuwa muungano unaoongozwa na Saudi Arabia umeshambulia kwa mabomu shule nchini Yemen, na kukiuka sheria za kimataifa za kiutu na kuzuwia maelfu ya watoto kupata elimu. Shirika hilo lenye makao yake makuu mjini London limeyataka mataifa yote ambayo yanaupatia silaha muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia , ikiwa ni pamoja na Marekani na Uingereza, kusitisha upelekaji...
WAZIRI wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, amewasilisha rasimu ya mkataba mpya kwa wajumbe katika mkutano mkuu unaojadili kuhusiana na mabadiliko ya tabia nchi mjini Paris, kwa usiku wa pili wa majadiliano. Fabius amesema kwamba lengo lao kuu ni kuhitimisha mazungumzo kwa dhima, sheria, matarajio,na makubaliano ya haki na ya kudumu mpaka kufikia leo, nakuongeza kusema kwamba wajumbe wa mkutano huo wanakaribia kufikia makubaliano ya mwisho. Awali, mkurugenzi wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachojishughulisha na mazingira, Achim...
UONGOZI wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam umekamilisha zoezi la kuapishwa kwa Madiwani wa Wilaya hiyo, zoezi ambalo limefatiwa na upigaji kura za kupata Meya pamoja na Naibu Meya wa Manispaa hiyo. Katika zoezi hilo ambalo limefanyika siku ya jana Addallah Chaulembo wa CCM amefanikiwa kushinda nafasi ya kuwa Meya wa Manispaa ya Temeke wakati Hassan Feisal wa CCM amechaguliwa kuwa Naibu Meya. Mara baada ya kuchaguliwa Meya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Chaulembo amesema wananchi...