MKUTANO wa baraza la Madiwani wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam umelazimika kuvunjika kufatia vurugu zilizojitokeza kutokana na baadhi ya wabunge na Mdiwani wa Zanzibar wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi-CCM- kuingia katika kikao hicho jambo ambalo vyama vya UKAWA vimepinga. Mkurugenzi wa Manispaa ya hiyo Mussa Natti amesema ameahirisha kikao hicho hadi hapo ufafanuzi wa kisheria juu ya Wabunge hao utakapopatikana. Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibamba John Mnyika amesema kitendo hicho cha...
Mabingwa wa Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo watakutana na timu ya Sanfrecce Hiroshima kutoka Japan hatua ya robofainali fainali za Kombe la Dunia la Klabu Jumapili. Washindi wa ligi ya Japan Sanfrecce Hiroshima wamelaza mabingwa wa Oceania Auckland City 2-0 leo kwenye mechi iliyochezewa Yokohama. TP Mazembe watua Japan kupigania ubingwa Mshindi wa mechi kati ya Mazembe na Hiroshima atakutana na mabingwa wa Amerika Kusini River Plate ya Argentina nusufainali Desemba...
Mchezaji wa kimataifa wa Honduras Arnold Peralta apigwa risasi na kufa wakati akiwa mapumzikoni kwenye mji wake wa nyumbani. Mauaji hayo yametokea kwenye maegesho ya magari katika eneo la maduka huko La Ceiba kwenye ufukwe wa Caribbean ambapo chanzo cha uvamizi huo hakijawekwa wazi. Kiungo huyo mwenye miaka 26 anaeichezea klabu ya Olimpia kwenye jiji kuu la Tegucigalpa Taifa hili la Honduras linatajwa kuwa moja ya nchi za viwango vya juu vya makundi ya uhali duniani. Osman Madrid mkurugenzi wa...
MPIGANAJI wa mwisho kati ya wapiganaji 11 wa Taliban ambao waliuzingira uwanja wa ndege wa Kandahar, Afghanistan ameuawa, zaidi ya saa 24, baada ya shambulizi kuanzishwa. Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan imesema leo kuwa watu 50 wakiwemo raia na maafisa wa usalama, wameuawa. Shambulizi hilo ambalo ni kubwa dhidi ya kambi ya jeshi la anga nchini humo, lilifanyika sambamba na mkutano wa kikanda nchini Pakistan, ambako Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan aliitaka Pakistan kusaidia kuanzisha tena mazungumzo ya...
VIONGOZI kadha kutoka eneo la Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya, wamekamatwa na polisi kuhusiana na madai ya kuwepo kwa makaburi yaliyozikwa miili ya watu kadha. Seneta Billow Kerrow amekamatwa pamoja na wabunge wengine wanne baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Wilson, Nairobi na kupelekwa makao makuu ya uchunguzi upande wa akosa ya...
SERIKALI ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ime amua kuingiza baadhi ya mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu katika sheria za Tanzania ili kuimarisha ulinzi wa haki za binadanu . Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es alaamu na makamu wa rais Mheshimiwa SAMIA SULUHU HASSAN wakati wa maadhimisho ya nane ya kitaifa na siku ya haki za binadamu duniani. Mheshimiwa SAMIA pia amewataka watanzania kuanzisha kampeni maalumu za kukuza maadili katika ngazi mbalimbali zikiwemo zile za utumishi wa umma...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta John Pombe Magufuli leo ametangaza rasmi Baraza la Mawaziri lenye Wizara 18 ambazo zitakuwa na Jumla ya Mawaziri 19. Baraza hilo limeonekana kuwa na mabadiliko makubwa ya Wizara na sura Mpya nyingi za Mawaziri ambao wataanza kulitumikia Taifa kwa miaka mitano. Akitangaza Baraza hilo mheshimiwa Magufuli amesema kwamba lengo kubwa la kuteua baraza dogo la Mawaziri ni kuhakikisha kuna kuwa na nidhamu ya matumizi ya...
MEXICO imekuwa nchi ya kwanza duniani kuruhusu matumizi ya chanjo ya kukinga maradhi ya homa ya denge yanayowasibu karibu watu Milioni mia moja kila mwaka duniani, na hasa katika nchi za joto. Idara kuu ya tiba nchini Mexico imesema chanjo hiyo ilifanyiwa majaribio kwa wagonjwa zaidi yaelfu 40,000 katika sehemu mbalimbali za dunia. Virusi vya homa ya denge husababisha mvujo wa damu wa ndani kwa ndani na kushindwa kwa viungo kufanya kazi. Virusi hivyo vinaenezwa na mbu....
WAKAZI wa mtaa wa Ibanda kata ya kirumba Jijini Mwanza wanatarajiwa kupokea mradi wa uwekaji Alama katika maeneo yao ili kupunguza migogoro ya Ardhi iliyokithiri katika kata yao. Hayo yamekuja mara baada ya mtaa huo kuwa na migogoro ya ardhi ya mara kwa mara na kuwaathiri wananchi waishio katika maeneo hayo. Mwenyekiti wa mtaa huo Ephrahim Nkingwa amesema tayari amewasilisha barua kwa mkurugenzi wa Jiji ya kuomba upimaji shirikishi ili kuhakikisha maeneo yote ya mtaa huo yanapimwa na kuepusha migogoro hiyo....
SERIKALI Mkoani Mara imeombwa Kuingilia kati nakuwachukulia hatua kali baadhi ya wazazi wanaopeleka watoto wa kike kukeketwa hususani katika kipindi hiki cha Tohara ambapo baadhi ya koo za kikurya tayari zimeanza Tohara suala ambalo linapelekea wanafunzi kuacha masomo. Hayo yamebainishwa na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kubitelele Robert Werema baada ya EFM RADIO, kutembelea shule hiyo ambayo inajumla ya wanafunzi 461, huku baadhi wakidawa kuwa wamepelekwa kwenye Tohara na sherehe za...