Slider

RAIS MAGUFULI APONGEZWA KWA KUHAMASISHA USAFI
Local News

BAADA ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwaongoza  Watanzania katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanganyika kwakufanya usafi jana, wanasiasa, wachambuzi na wananchi mbalimbali wamepongeza hatua hiyo na kuwataka watanzania kuitumia  kama mfano wa wao kuendeleza utamaduni huo wa kufanya usafi. Wakizungumza na Efm kwa nyakati Tofauti leo, wamesema kitendo cha usafi kilichofanyika jana kimewakumbusha uongozi wa enzi za Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye aliwashirikisha wananchi wote kwa kila hatua za...

Like
280
0
Thursday, 10 December 2015
ARSENAL YAILAZA  OLYMPIAKOS 3-0
Slider

Olivier Giroud alifungia Arsenal mabao matatu kwa mara yake ya kwanza na kuhakikisha Gunners wanaendeleza rekodi yao nzuri Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na kufika hatua ya 16 bora kwa kulaza Olympiakos. Arsenal walihitaji kushinda kwa mabao mawili wazi lakini walipata mabao hata zaidi na kumaliza wa pili Kundi F. Giroud alianza kwa kufunga kwa kichwa kipindi cha kwanza, kisha akafunga la pili kipindi cha pili kwa usaidizi kutoka kwa Joel Campbell. Mfaransa huyo alihakikisha Arsenal wanafuzu kwa kufunga la...

Like
301
0
Thursday, 10 December 2015
EFM, DTB BANK, BONGO MOVIE NA HALMASHAURI YA WILAYA YA KINONDONI WAKIFANYA USAFI SIKU YA UHURU
Local News

E-fm na DTB Bank kwa kushirikiana na na Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mh. Paul Makonda pamoja na waigizaji wa Bongo Movie na wananchi wa wilaya ya Kinondoni  leo wametekeleza agizo la Rais Mh. John Pombe Mgufuli  kwa kuitumia siku ya maadhimisho ya uhuru kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya nchi. Usafi huu ulianzia eneo la Kinondoni Moroco hadi magomeni ambapo Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu pia alijumuika kufanya usafi ikiwa ni pamoja na...

Like
952
0
Wednesday, 09 December 2015
SHAMBULIO LA NDEGE YA MAREKANI LAUA KIONGOZI WA AL SHABAAB
Global News

KONGOZI mmoja wa kundi la Al Shabaab ameuawa katika shambulizi la ndege ya Marekani. Msemaji wa makao makuu ya ulinzi ya Marekani Peter Cook amesema kifo cha Abdirahman Sandhere ni pigo kubwa kwa usimamizi na uwezo wa mashambulizi ya kundi hilo linalounga mkono wanamgambo wa Al Qaeda. Al Shabaab inaendesha kampeini ya kuing’oa madarakani serikali inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa inayoundwa na zaidi ya majeshi Elfu 22 wa umoja wa Afrika....

Like
273
0
Tuesday, 08 December 2015
ETHIOPIA YAONYWA KUKUMBWA NA BALAA LA NJAA
Global News

SERIKALI ya Ethiopia imeonya kuwa watu milioni 10 wanakabiliwa na janga la njaa kufuatia ukame mkubwa uliokumba maeneo mengi nchini humo. Ukame huo umekadiriwa kwamba utaathiri takriban watoto milioni 6 ambao watahitaji msaada wa chakula kuanzia mwezi ujao. Hata hivyo tayari Serikali imeanza kugawa chakula cha msaada kwa ushirikiano na mpango wa chakula duniani WFP kufuatia ukame ulioathiri mazao katika kipindi cha msimu...

Like
275
0
Tuesday, 08 December 2015
JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA KUFANYA USAFI MANISPAA YA ILALA
Local News

JUMUIYA ya Wafanyabiashara Tanzania inatarajia kufanya usafi wa Mazingira katika baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Ilala ikiwa ni hatua ya kuunga mkono Agizo la Rais Dokta John Pombe Joseph Magufuli la kufanya usafi siku hiyo. Akizungumza  na Wanahbari jijini Dar es salaam Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Jeddah Hasabubaba amewataka Wafanyabiashara wote wa Jumuiya hiyo kujitokeza na kushiriki kufanya usafi wa mazingira. Aidha Hasabubaba ameongeza kuwa suala hilo halitokuwa suala la siku moja bali ni endelevu na kuwa wanaunga...

Like
420
0
Tuesday, 08 December 2015
MAFUNZO YAKUKABILIANA NA MIONZI YA NYUKLIA YATOLEWA NCHINI
Local News

TUME ya Nguvu za Atomiki, Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani wanaendeshesha mafunzo ya namna ya kukabilina na matukio ya mionzi hatari yenye lengo la kutoa mwongozo jinsi ya kukabiliana na majanga yanayoweza kusababishwa na mionzi hatari ya nyuklia. Akifungua mafunzo hayo Jijini Arusha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki nchini dokta Mwijarubi Nyaruba amesema kutokana na kukua kwa kasi kwa teknolojia duniani ni muhimu kwa nchi wanachama wa shirika la nguvu za...

Like
227
0
Tuesday, 08 December 2015
RUSHWA: MAHAKIMU 20 WAFUKUZWA KAZI GHANA
Global News

MAMLAKA ya mahakama nchini Ghana imewafuta kazi mahakimu 20 huku wengine wakiendelea kuchunguzwa kutokana na kuhusishwa na kashifa ya kupokea rushwa. Ufisadi wa mahakimu hao umebainika baada ya mwandishi wa habari za uchunguzi, Aremeyaw Anas, kukusanya kwa muda wa miaka miwili kanda za video zenye muda wa saa 500 kama ushahidi dhidi ya mahakimu 30. Kutokana na sakata hilo, baadhi ya mahakimu nchini Ghana wametaka kuwepo kwa mabadiliko katika mahakama nchini humo ili kukomesha vitendo...

Like
209
0
Tuesday, 08 December 2015
BURUNDI KUJADILIWA BRUSSELS LEO
Global News

MKUTANO wa ngazi za juu wa kujadili hali nchini Burundi utaanza leo mjini Brussels, Ubelgiji huku mada kuu ikiwa ni msukosuko wa kisiasa nchini humo na uhusiano wake na Umoja wa Ulaya. Mkutano huo, ambao utashirikisha viongozi wa ngazi za juu kutoka mataifa ya Afrika Mashariki, unafanyika kutokana na Umoja wa Ulaya kukusudia kuiwekea vikwazo vya kibiashara nchi ya Burundi. Umoja wa mataifa umesema kwamba kufuatia Burundi kushindwa kuheshimu vipengele muhimu katika mkataba wa ushirikiano umoja huo unatarajia kuanzisha utaratibu...

Like
200
0
Tuesday, 08 December 2015
NEMA FOUNDATION YATOA MSAADA WA MASHUKA KATIKA BAADHI YA HOSPITALI DAR
Local News

TAASISI isiyo ya kiserikali ya- NEMA FOUNDATION imetoa msaada wa mashuka miamoja katika  baadhi ya hospitali  za Jijini Dar es salaam ikiwemo hospitali ya Mwananyamara ikiwa  ni sehemu  ya utaratibu wao ambao wanaufanya kila mwaka. Mwenyekiti wa Taasisi hiyo  Bi Mariam  Dedes amesema kuwa wameguswa kutoa misaada hiyo kwa kutambua changamoto mabalimbali zinazo ikabili sekta ya Afya. Kwa upande wake Mbunge wa kinondoni Muheshimiwa  Mahulid  Mtulya ameishukuru taasisi hiyo na kuziomba taasisi nyingine kujitokeza kutoa misaada kwenye ...

Like
280
0
Tuesday, 08 December 2015
ZAIDI YA ASILIMIA 15 YA WANAWAKE NCHINI HUFANYIWA VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KIJINSIA
Local News

IMEELEZWA  kuwa zaidi ya asilimia  15 ya wanawake  nchini wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia . Hayo yamebainishwa jana Jijini  Dar es alaamu  na mkuu wa program  wa mtandao wa jinsia  TGNP  Sikola  Makwaiya  wakati wa  maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili  wa  kijinsia  ambapo amesema zaidi ya wanawake Elfu 15 nchini  sawa na asilimia 15 hukumbwa na vitendo vya unyanyasaji wa kijimsia. Makwaiya  ametaja baadhi ya mikoa inayoongoza  kwa vitendo hivyo kuwa ni  Shinyanga, Mara na...

Like
281
0
Tuesday, 08 December 2015