MGOMBEA Urais kupitia chama cha upinzani cha Conservative Mauricio Macri amethibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Argentina huku mgombea wa chama tawala akikubali kushindwa. Matokeo yaliyotangazwa yameonesha Macri amepata asilimia 52 ya kura zote zilizopigwa huku mgombea wa chama Tawala Daniel Scioli akipata asilimia 48. Hata hivyo katika Uchaguzi wa awamu ya kwanza uliofanyika mwezi Oktoba Macri ambaye ni meya wa zamani wa Buenos Aires, alikuwa ameshindwa na Scioli ambaye ni gavana wa mkoa wa Buenos Aires....
UBELGIJI imesema kuwa imewakamata watu 16 katika operesheni ya polisi ya kupambana na ugaidi mjini Brussels. Katika msako huo, nyumba kumi na tisa zimekaguliwa, ingawa hakuna silaha zilizokamatwa. huku mtuhumiwa mkuu wa shambulio lililotokea mjini Paris, Salah Abdeslam, bado hajakamatwa. Operesheni hiyo ya polisi kuhusiana na tishio la ugaidi mjini Brussels imemalizika bila kupatikana kwa vithibitisho vya kutosha kwa wahusika hali iliyosababisha mamlaka ya mji huo kuongeza muda ili kufanya uchunguzi Zaidi wa tukio...
KUTORATIBIWA kwa mbegu za Alizeti na ukosefu wa mitaji umeelezwa kuwa changamoto kubwa kwa wasindikaji wadogo wa mafuta ya mbegu ya alizeti katika uendeshaji wa viwanda. Hayo yameelezwa na Wakala wa uendelezaji Kongano la Mafuta ya Alizeti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo la Viwanda (UNIDO) Vedastus Timothy wakati akizungumza na waandishi wa habari walioambatana na Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez. Timothy amesema kwamba pamoja na kuwepo kwa taarifa za...
WANAFUNZI wenye mahitaji maalum wanaosoma vyuo vikuu nchini wameaswa kutumia elimu wanayoipata ili kuendesha maisha yao na kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla. Hayo yamesemwa na Mgeni rasmi wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaama (DUCE) Profesa Martha Qorro yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es salaaam. Profesa Qorro amesema kuwa mwamko wa wanafunzi wenye mahitaji maalum kujiunga na elimu ya juu nchini ni mzuri licha ya changamoto zinazowakumba...
Mchezaji tenisi namba moja Duniani kutoka Serbia, Novak Djokovic amemaliza msimu wake kwa ushindi dhidi ya Roger Federer. Ushindi huo umemfanya kuweka rekodi ya taji la nne mfululizo la mashindano ya ATP. Djokovic alifanikiwa kushinda kwa seti 6-3, 6-4 katika dakika 80 za mchezo huko London, na aliweza kusahihisha makosa yake baada ya mechi ya mwanzo ya makundi kufungwa na Roger Federer. Mpaka sasa Djokovic anamaliza mwaka huu kwa kushinda mataji 11 yakiwemo ya matatu ya Gland slam, na kwa...
Kocha wa Manchester United imethibitishwa anajaribu kumrejesha mshambuliaji matata wa Real Madrid Cristiano Ronaldo Old Trafford . Louis van Gaal amethibitisha kuwa wanawafuatilia wachezaji kadhaa akiwemo Ronaldo kwa nia ya kuwarejesha Old Trafford ilikuiimarisha ushindani wake msimu huu. ”Kwa hakika tunawafuatilia wachezaji kadhaa sio tu Ronaldo.” ”Kwa kiwango kikubwa wengi wa wachezaji tunaowataka hawaachiki” ”Kumhusu Ronaldo, kwa hakika tunasubiri thibitisho kwa udi na uvumba” alisema Van Gaal....
Dakika 90 za mtanange wa mpira wa miguu kati ya E-fm Vs Tabata Veterani zilimalizika kwa sare ya bila kufungana. Burudani hii ya mpira ilishuhudiwa na mamia ya wakazi wa Tabata waliovutiwa kuona wafanyakazi wa Efm wakiwemo Rdj’s na watangazaji wakisakata kabumbu. Kikosi cha E-fm chini ya kikiongozwa na nahodha wake Ssebo kwenye picha ya pamoja Picha ya pamoja ya Tabata Veterani Mpira ukiendelea katika uwanja wa shule ya Msingi Tabata E-fm wakiliandama lango la Tabata Veterani Mashabiki wa...
MWILI wa mshukiwa wa 3 wa kosa la kigaidi umepatikana katika nyumba ya Saint-Denis iliovamiwa na maafisa wa polisi kuhusiana na shambulizi la Paris, kulingana na kiongozi wa mashitaka nchini humo. Vilevile amethibitisha kuwa mwanamke mmoja ni miongoni mwa watu watatu waliouawa, huku pasipoti ilio na jina la Hasna Aitboulahcen ilipatikana kwenye begi lake katika eneo hilo. Hata hivyo Mwili mmoja umetambulika kuwa wa kiongozi wa shambulio hilo Abaaoud...
WATU wenye silaha wameshambulia hoteli ya Radisson Blu katika mji mkuu wa Mali, Bamako. Ripoti zinaeleza kwamba Kuna dalili kwamba hilo ni jaribio la kuwachukua watu mateka ambapo Milio ya risasi imesikika kutoka nje ya hoteli hiyo. Hata hivyo Maafisa wa usalama wa serikali ili kupata usaidizi kurejesha usalama na hali ya kawaida hotelini hapo pamoja na wananchi wote walio karibu na maeneo hayo. sehemu ya...
RAIS wa Ireland, Michael Higgins amemtumia Salamu za Pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya Tano. Katika Salamu zake hizo, Rais Higgins amesema Ireland na Tanzania zimekuwa na uhusiano mzuri na wa kirafiki kwa miaka mingi, hivyo ana matarajio kwamba katika kipindi cha uongozi wa Rais Magufuli, uhusiano huo utaimarishwa zaidi. Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mheshimiwa Robert Mugabe amemtumia Salamu za...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli amelihutubia Bunge la Tanzania ikiwa ni mara ya kwanza kulihutubia na kulifungua rasmi Tangu aingie Madarakani. Katika hotuba yake Rais Magufuli ameeleza mikakati yake na vipaumbele vyake vitakavyowaletea maendeleo wananchi pamoja na Taifa kwa ujumla na mwelekeo wa kiuchumi. Kabla ya kulihutubia Bunge Rais Magufuli leo asubuhi amemwapisha rasmi Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano mheshimiwa Majaliwa Kassim...