KANSELA wa Ujerumani Angela Merkel amesema mzozo wa wahamiaji unaolikumba bara la Ulaya utasuluhishwa katika mipaka ya nje ya Umoja wa Ulaya na mbali ya mipaka hiyo. Akizungumza akiwa na Kansela wa Austria Werner Faymann, Merkel amesema Ulaya inahitaji uimara na kasi zaidi kuhusu kushughulikia maeneo yaliyo na utata ikiwemo Ugiriki ambako wakimbizi na wahamiaji wanaweza kusajiliwa. Ujerumani imeshuhudia ongezeko la wahamiaji huku ikiwapokea zaidi ya wahamiaji laki saba hadi kufikia mwezi...
RAIA nchini New Zealand leo wanapiga kura kuchagua bendera ya Taifa ambayo huenda ikachukua nafasi ya bendera ya sasa. Kura hiyo ya maamuzi inapigwa kuanzia leo hadi Desemba 11 kupitia posta kuamua bendera moja kati ya tano zilizopendekezwa ambayo ni bora zaidi. Waziri Mkuu wa nchi hiyo John Key amesema bendera ya sasa haiakisi hali halisi ya New Zealand na kuamini kuwa bendera hiyo inafanana na bendera ya...
USHIRIKIANAO mdogo kati ya wazazi, walimu na wanafunzi mkoani TABORA umetajwa kuwa ni sehemu ya vikwazo vya kimaendeleo ya elimu ya msingi mkoani humo. Hayo yamebainishwa na wadau mbalimbali wa elimu mkoani TABORA walioshiriki mdahalo wa masuala ya elimu uliohoji anguko la elimu mkoani humo. Moja ya vitendo vilivyotajwa kufanywa na wazazi ni pamoja na kuwepo kwa hisia za vitendo vya kishirikina hali inayotajwa kukimbiza walimu wengi wanaopangwa kufundisha shule za msingi mkoani...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli amemuapisha Waziri Mkuu Mteule wa Serikali ya awamu ya Tano Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa Ikulu Ndogo iliyopo Chamwino Mkoani Dodoma ambapo baadaye pia atalihutubia Bunge la Tanzania. Viongozi mbalimbali wameshirki katika Zoezi la kumuapisha Waziri Mkuu Mteule akiwemo makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo Watanzania wengi wanatarajia kusikia mikakati ya Mheshimiwa Rais dokta Magufuli atakayoitekeleza ikiwemo aliyowaahidi wakati wa Kampeni...
MISIKITI iliyopo nchini Marekani na Canada inakabiliwa na ongezeko la uharibifu na vitisho vya kigaidi tangu kutokea kwa shambulio kali mjini Paris. Vituo vya kiislamu vimekuwa vikipokea ujumbe wa chuki katika simu huku baadhi ya misikiti ikichapishwa michoro ya moto na jumbe za kulipiza kisasi. Hata hivyo Nchini Canada, mtu mmoja aliyekuwa amejifunika uso wake amekamatwa na maafisa wa polisi baada ya kutishia kuwaua waislamu huko Quebec na kutishia kumuua mwarabu mmoja kila...
BASI moja lililokuwa likisafiri kutoka mjini Juba kuelekea kampala nchini Uganda limevamiwa na kufyatuliwa risasi leo majira ya saa moja asubuhi. Maafisa wa Polisi wa Sudan Kusini wameeleza kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la Moli takribani kilomita 50 kutoka mji wa mpakani wa Nimule na kwamba kwa sasa bado wanaendelea kutafuta idadi kamili ya watu waliojeruhiwa. Hata hivyo maafisa hao wamebainisha kwamba wanafanya jitihada za kukutana na kujadiliana na wenzao wa Uganda ili kubaini chanzo cha tukio...
SERIKALI imetakiwa kuhakikisha inatunga na kuboresha sera za kupambana na ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake katika masoko na maeneo mbalimbali nchini. Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Kituo cha Usuluhisho cha Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania-TAMWA, Gladness Munuo wakati kizungumza kwenye semina ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara wa soko la Ilala juu ya namna ya kutoa habari za unyanyasaji wa kijinsia kwa waandishi wa habari. Aidha MUNUO ameeleza kuwa mifumo dume ya uongozi nchini imekuwa haitoi...
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepokea na kuthibitisha Uteuzi wa jina la Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya Tano ambaye ni mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Mkoani Lindi kupitia chama cha mapinduzi-CCM. Akitangaza jina hilo Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai amewaeleza wabunge kuwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa Rais Mamlaka ya kuteua jina la Waziri Mkuu na kuliwasilisha bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na wabunge. Mheshimiwa...
254: Wakati Sauti Sol wanajiandaa kushusha albam yao “LIVE AND DIE IN AFRICA” Followers wa mrembo Huddah wamefunguka vikali kwenye ukurasa wa instagram wa mrembo huyu baada ya kuweka post ya kumtakia heri ya kuzaliwa rafiki yake anaetajwa ku jihusisha na mapenzi ya jinsia moja, comment hizo zimemtaka Huddah kufuta post hiyo lakini pia mlengwa wa hiyo post ametakiwa kufuta akaunti yake ya Instagram na kubadilika. Post hiyo ya Huddah inaonyesha dhahiri kuwa yeye binafsi anasapoti kitu kinachofanywa na rafiki...
RAIS wa Sudan kusini Salva Kiir amesisitiza nia yake ya kuendeleza makubaliano ya Amani yaliyotiwa saini mwezi Agosti, siku mbili baada ya serikali na waasi kushutumiana kwa kukiuka makubaliano hayo. Rais Kiir ameliambia bunge la nchi hiyo kwamba Sudan kusini inapaswa kufikia maridhiano na kufungua kurasa mpya na kuitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia nchi hiyo kutekeleza makubaliano ya amani. Mvutano wa kuwania madaraka kati ya rais Salva Kiir na ...
WAPIGANAJI wa Islamic State (IS) wamethibitisha kuwaua mateka wawili, ambao ni raia wa Norway na raia wa China. Waziri mkuu wa Norway Erna Solberg amesema hakuna sababu zozote za kutilia shaka tangazo la wapiganaji hao na kutaja kitendo chao kuwa ni “unyama”. Naye Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Hong Lei amesema kwamba tangu raia huyo nchi yake akamatwe, Taifa hilo limefanya jitihada za kumuokoa bila...