Slider

CHAMA CHA PTF MASHUJAA CHAPATA USAJILI WA MUDA
Local News

CHAMA cha Tanzania Patriotic Front-TPF-MASHUJAA kimepata usajili wa muda kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa wakati kikijiandaa kupata usajili wa kudumu kwa kuzingatia na kutimiza mashari na sheria ya usajili wa vyama vya siasa nchini.   Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam baada ya usajili wa chama hicho Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa chama hicho kutambua kuwa chama ni kwa ajili ya wanachama na si kwa jili ya maslahi ya viongozi wa...

Like
332
0
Monday, 09 November 2015
MKUTANO WA PILI WA AMANI NA USALAMA AFRIKA KUFANYIKA DAKAR
Global News

MKUTANO wa Awamu ya pili wa Amani na usalama barani Afrika unatarajia kufanyika mjini Dakar nchini Senegal kwa muda wa siku mbili zijazo. Mkutano huo utawasaidia viongozi wa nchi, mawaziri na wataalamu wa jeshi kuangalia njia bora za kuimarisha usalama na utulivu barani Afrika. Aidha Mkutano huo wa kimataifa wa awamu ya pili unalenga zaidi changamoto za bara la Afrika na athari zake katika ngazi za...

Like
302
0
Monday, 09 November 2015
UPINZANI WAELEKEA KUSHINDA UCHAGUZI CROATIA
Global News

CHAMA cha upinzani nchini Croatia kinaelekea kupata ushindi kwenye uchaguzi wa ubunge uliofanyika Jumapili ya wiki iliyopita ingawa bado hakijapata viti vya kutosha kuunda serikali. Matokeo ya awali yanaonyesha chama hicho cha -HDZ-kitapata viti 60, huku muungano unaotawala wa Social Democrats wa waziri mkuu anayeondoka Zoran Milanovic ukipata viti 50. Hata hivyo Chama hicho cha wahafidhina sasa kinatarajiwa kuanza mazungumzo ya kuunda...

Like
264
0
Monday, 09 November 2015
SIMANJIRO: MADIWANI WATEULE WATAKIWA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI BILA UCHOCHEZI
Local News

MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amesema atawachukulia hatua kali, baadhi ya madiwani wateule wa wilaya hiyo ambao watasababisha vurugu na kuchochea migogoro kwa wananchi. Kambona ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Loiborsoit A, kata ya Emboreet, ambapo amewataka madiwani hao watatue migogoro ya Ardhi bila kuathiri usalama uliopo kwa watu. Aidha amewataka viongozi hao kutowashawishi wananchi na kusababisha vurugu badala yake watumie hekima na busara kutatua migogoro ya ardhi...

Like
340
0
Monday, 09 November 2015
MAKTABA NCHINI KUJENGEWA UWEZO
Local News

BODI ya huduma za maktaba nchini-TLSB-imeanzisha mradi wa Maktaba kwa maendeleo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 630 ili kuzijengea uwezo wa utendaji kazi bora maktaba zote nchini. Akizungumza katika mradi huo Mkurugenzi mkuu wa-TLSB-dokta Ali Mcharazo amesema Mradi huo ambao utatumia zaidi teknolojia ya habari na Mawasiliano-(Tehama)-kwa kutumia maktaba zinazohamishika, utawafikia walengwa moja kwa moja katika maeneo yao ya uzalishaji na kuwawezesha kupata taarifa muhimu za kuendeleza shughuli zao za kila siku. Kwa Upande wao...

Like
247
0
Monday, 09 November 2015
SAMATTA MFUNGAJI BORA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA
Slider

Klabu ya soka ya TP Mazembe, ya Jamuhuri ya Kidemocrasia ya Congo imetwaa ubingwa wa klabu bingwa barani Afrika. TP Mazembe wakicheza kwao katika uwanja wa Stade du TP Mazembe Lubumbashi, waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi Union Sportive Medina d’Alger. Mshambuliaji Mbwana Samatta ndiye aliyeanza kuifungia timu yake bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 75 ya mchezo, kisha Roger Assale akahitimisha kazi kwa bao la pili katika dakika ya 90. Mazembe imenyakua Ubingwa huu...

Like
448
0
Monday, 09 November 2015
PICHA: MUZIKI MNENE BAR KWA BAR 2015 SMART PARK
Entertanment

Rdj Con Rdj Manz Rdj Skit Rdj...

Like
320
0
Saturday, 07 November 2015
E-FM VS KILUVYA VETERANI 2-1
Slider

Mechi ya Mpira wa miguu kati ya E-fm Vs Kivule Veterani imemalizika huku E-fm ikiruhusu washambuliaji wa Kivule Veterani kuziona nyavu mara mbili huku Efm wakiliona lango lao mara moja kupelekea matokeo kuwa 2 – 1, na ushindi kwenda Kivule Veterani wakiutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani Watangazaji wa vipindi vya Sports Headquarters na E Sports, Sud Mkumba na Oscar Oscar wakizungumza na mashabiki kabla ya kushuka dimbani. Picha ya pamoja ya kikosi cha E-fm Kikosi cha timu ya Kivule...

Like
482
0
Saturday, 07 November 2015
LIBYA: MAKUNDI HASIMU  YAMETAKIWA KUTOKWAMISHA MIPANGO YA KUGAWANA MADARAKA
Global News

MJUMBE  wa  Umoja  wa  Mataifa  nchini  Libya  ambaye anaondoka  ameyataka  makundi  hasimu  nchini  humo  kusitisha  juhudi  zao  za  kuzuwia  mpango  wa kugawana  madaraka unaolenga  katika  kumaliza  mzozo wa  kisiasa  nchini  mwao. Bernardino  Leon, ambaye  nafasi  yake  inatarajiwa kuchukuliwa  hivi  karibuni  na  mwanadiplomasia  wa  siku nyingi  wa  Ujerumani,  Martin Kobler, pia  amejitetea  dhidi ya  maelezo  kwamba  kuna  mvutano  wa  kimaslahi kwake  kukubali  kazi  katika  Umoja ...

Like
327
0
Friday, 06 November 2015
MISRI YAZUIA NDEGE ZA SHIRIKA LA UINGEREZA
Global News

SERIKALI ya Misri imesimamisha safari za shirika la ndege la Easyjet ambalo lilikuwa limepangiwa kuwasafirisha baadhi ya Waingereza waliokwama mji wa Sharm el-Sheikh leo.   Ndege za shirika la Easyjet pamoja na ndege za mashirika ya Monarch, Thomson na British Airways ndizo zilizokuwa zimepangiwa kuwasafirisha Waingereza waliokuwa Sharm el-Sheikh baada ya Uingereza kusitisha safari za ndege za kuingia na kutoka katika mji huo.   Hatua hii imekuja  baada ya kuibuka kwa uwezekano kwamba huenda ndege ya Urusi iliyoanguka baada ya...

Like
234
0
Friday, 06 November 2015
VIJANA WANAOJIUNGA NA JKT KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI
Local News

BARAZA la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi NEEC  kwa kushirikiana na jeshi la kujenga  taifa JKT limeanzisha program ya  kutoa mafunzo ya  mtaala maalumu kwa ajili ujasiriamali na uendeshaji wa biashara kwa  vijana wanaojiunga na  jeshi  hilo   kwa kujitolea.   Vijana  hao  ambao hawapati ajira wanafikia  elfu 2,hivyo NEEC imeamua kuwaendeleza  kutokana na  mafunzo  ya  elimu za stadi  za maisha wanayopata  wawapo jeshini  kwa kipindi chote cha miaka miwili...

Like
352
0
Friday, 06 November 2015