JUMLA ya watu 27 walioripotiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa kipindupindu Jijini Arusha kati yao 6 wamethibitishwa kuwa na ugonjwa huo ambapo hadi sasa watano wamelazwa katika kituo cha Afya cha Levolosi. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkurlu amewataka wakazi wa Jiji la Arusha kufuata kanuni Afya ili kuepuka ugonjwa. Nkurlu amesema kuwa kwa zaidi ya miezi miwili sasa maeneo mbali mbali nchini yameripotiwa kuwa na ugonjwa huo ikiwemo mikoa ya...
WIZARA ya Maliasili na Utalii imefanikiwa kutoa ajira mpya kwa Watumishi wapya 588 katika kitengo cha Afisa Wanyamapori na Wahifadhi wanyamapori lengo ikiwa ni kukabiliana na tatizo la kuenea kwa vitendo vya ujangili kwa wanyama. Akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo elekezi kwa waajiriwa hao jana katika Chuo cha Taifa cha Utalii Kampasi ya Temeke jijini Dar es Salam, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, dokta Adelhelm Meru amewashauri watumishi kujituma zaidi ili kukidhi malengo yaliyowekwa. Mbali na hayo amewataka...
WAZIRI wa Ulinzi wa Marekani Ashton Carter amesema Marekani inapanga kuimarisha mashambulizi yake ya anga dhidi ya kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu nchini Iraq na Syria. Akizungumza mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu masuala ya ulinzi, waziri Carter amewaambia maseneta kuwa majeshi ya Marekani yatailenga miundo mbinu ya mafuta inayomilikiwa na kundi hilo na pia kuimarisha mafunzo ya wanajeshi wa mataifa ya Kiarabu wanaopambana ardhini na wanamgambo wa IS. Marekani na Urusi zina malengo yanayokinzana katika eneo hilo,...
MKUTANO mKuu wa Umoja wa Mataifa umeunga mkono kwa kauli moja azimio linalotoa wito kwa Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya Cuba. Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilipata kura 191 dhidi ya 2 kulaani vikwazo vya kibiashara, kiuchumi na kifedha ambavyo Marekani imeliwekea taifa hilo la kikomunisti. Hata hivyo ingawa kura hizo zilipigwa bado Marekani ilipiga kura ya kupinga azimio hilo la Vikwazo vilivyowekwa tangu mwaka 1960, wakati wa kilele cha Vita Baridi, Marekani ilipovunja mahusiano yake na...
WAKATI Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini-NEC-ikiendelea na Zoezi la kuhesabu kura, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi-UKAWA- vimeendelea kupinga Matokeo na kuiomba Tume hiyo kusitisha zoezi hilo kwa madai kuwa zoezi hilo halitendi haki kwa vyama vya upinzani. Hayo yamebainishwa leo na Mgombea wa nafasi ya Uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaeungwa mkono na –UKAWA- Edward Lowasa wakati akizungumz na Waandishi wa habari ambapo amesema ni vyema Tume kuanza upya zoezi hilo kwa kutumia karatasi zilizosainiwa...
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Salim Jecha Salim ametangaza kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi visiwani humo kwa kudai kuwa uchaguzi huo ulijaa kasoro nyingi. Akizungumza kupitia Televisheni ya serikali ya Visiwani Zanzibar-ZBC-Jecha amesema kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki na kwamba kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi. Aidha amesema kuwa ukiukwaji huo umetokana na baadhi ya makamishna wa Tume hiyo, kutotekeleza majukumu yao kama inavyotakiwa...
WANAHARAKATI wa kutetea Haki za Binadamu wamezionya shule za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC, kutowaandikisha watoto wa shule hizo kujiunga jeshini. Kundi la wanaharakati hao lenye makao yake makuu nchini Marekani limesema kuwa makundi yenye silaha yamekuwa yakiwateka wanafunzi katika majimbo ya Kivu ya kaskazini na kusini na kuwalazimisha kujiunga na Jeshi. Katika ripoti yake, kundi hilo pia limeyalaumu makundi ya waasi na jeshi la serikali ya Congo, kwa kutumia shule kama kambi zake za kijeshi au kuhifadhia...
TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini Ivory Coast imemtangaza Alassane Ouattara kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini humo kwa ushindi wa asilimia 83.66. Raia wa Ivory Coast wameonesha kufurahishwa na ushindi wa Rais Alassane Outtara kama walivyotarajiwa kwamba rais huyo ataongoza kwa muhula mwingine wa miaka mitano. Baada ya mwongo mmoja wa kutoimarika kwa uchumi na vita vya wenyewe kwa wenyewe, wengi watafurahia kwamba uchaguzi huo ulifanyika kwa...
JUMLA ya watahiniwa 12,011 wa kidato cha nne Jijini Mbeya wanatarajiwa kuanza mtihani wa Taifa Novemba mbili mwaka huu, ikilinganishwa na wanafunzi 2,895 waliofanya mtihani huo mwaka jana. Hayo yamesemwa na Afisa habari wa halmashauri ya jiji la Mbeya kwa niaba ya Afisa Elimu sekondari Jaquline Msuya amesema kati ya watahiniwa hao wasichana ni 6373 na wavulana 5638. Kwa upande wake mkuu wa shule ya Sekondari ya Southern Highland ya jijini Mbeya Chamila Evarist amesema wamejiandaa vyema kuhakikisha wanafunzi wote...
TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini-NEC-imewataka wananchi kutopotoshwa na maneno ya wanasiasa juu ya matokeo ya nafasi ya Urais yanayotolewa na Tume hiyo kuwa yana upendeleo suala ambalo halina ukweli wowote. Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam leo kabla ya kuanza kutangaza matokeo, mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa Tume inatangaza matokeo kwa mujibu wa taratibu na namna yanavyoifikia. Mbali na hayo Jaji Mstaafu Lubuva ameviasa vyama vya siasa kutoendelea kuwapotosha watanzania kwani...
KUNDI linalopinga uhamiaji PEGIDA limehamasisha idadi kubwa ya watu wanaoliunga mkono katika mji wa mashariki nchini Ujerumani wa Dresden kujiunga na kundi hilo. Kwa mujibu wa kundi huru la wanafunzi linalofanya utafiti la Durchgezält, mkutano wa PEGIDA ulihudhuriwa na watu kati ya Elfu kumi hadi Elfu kumi na mbili. Lutz Bachmann, mmoja kati ya waasisi wa kundi hilo, alihutubia hadhara hiyo na kukosoa msimamo wa serikali ya kansela Angela Merkel, akidai imechukua...