KATIKA tukio la kusikitisha, mkazi wa kitongoji cha Songambele Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ameuawa kwa kukatwa katwa mapanga, baada ya kudai mtoto wake kwa mke wa mtu. Wakizungumza kuhusiana na tukio hilo baadhi ya mashuhuda wamedai kuwa marehemu huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi wa muda mrefu na mwanamke huyo ambaye ni mke wa mtu. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, kamishna msaidizi (ACP) Christopher Fuime amesema tukio...
MKUU wa jeshi la polisi Nchini ERNEST MANGU amevipongeza vyombo vya habari nchini kwa kazi kubwa wanayofanya kuelimisha jamii hususani katika habari zinazosaidia kuzuia uhalifu na kuhamasisha wananchi kudumisha amani kipindi hiki cha uchaguzi mkuu. IGP Mangu amewaambia wandishi wa habari kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea kumalizika kwa kampeni za uchaguzi mkuu hali ya nchi kwa ujumla imeendelea kuwa shwari na jeshi la polisi limeweza kudhibiti kwa kukemea na kuwafikisha mahakani watu wachache waliofanya vitendo vyenye uvunjifu wa...
MAKAMU wa Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kwamba hatawania urais mwaka ujao. Ni wazi sasa kuwa Bernie Sanders ndiye mpinzani mkuu wa Mama Hillary Clinton kwa uwaniaji wa Urais wa Marekani kupitia chama cha Democrat, baada ya Makamu wa Rais Joe Biden kutangaza kuwa hatagombea Urais wa Marekani. Akiongea katika mji mkuu wa New York, Bwana Sanders alimpongeza Makamu wa Rais kwa kutoa huduma muhimu kwa jamii kwa muda...
MAREKANI imeshutumu Urusi kwa kumpa mapokezi ya heshima Rais wa Syria Bashar al-Assad mjini Moscow. Afisa wa wizara ya masuala ya ndani ya Marekani amesema taifa hilo halijashangazwa na ziara hiyo, lakini wasiwasi mkubwa kwa Marekani ni Urusi kuendelea kumsaidia kivita Assad kitendo ambacho inaamini kuwa litaipa nguvu zaidi serikali ya Assad na hivyo kuendeleza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Ziara hiyo ya kiongozi wa Syria ilifanyika wiki tatu baada ya Urusi kuanza kushambulia kwa ndege ngome za...
VITENDO vinavyofanywa na baadhi ya vijana nchini vyakuweka bendera za vyama mbalimbali vya siasa katika nguzo na nyaya za umeme vimeelezwa kuwa vinahatarisha maisha yao. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mhandisi FELCHESMI MRAMBA ameimbia EFM kuwa ni wakati wa vijana kujithamini na kuthamini uhai wao badala ya kufanya vitu bila kufikiria athari zake...
KESI ya Kikatiba kuhusu tafsiri ya Umbali wanaotakiwa kusimama wapiga kura baada ya Kupiga kura Wakati wa Uchaguzi mkuu inasomwa leo na kutolewa maelekezo maalum baada ya hapo jana kuahirishwa. Akizungumza jana wakati anatoa maamuzi hayo mwenyekiti wa jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo JAJI SAKIETI KIHIYO ameleza kuwa baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili kuhusiana kesi hiyo jana, mahakama imetoa uamuzi wa kuahirisha kesi hiyo hadi leo ambapo watatoa maamuzi yenye maelekezo maalum kuhusu umbali ambao wapiga...
POLISI nchini Congo Brazaville wamefyatua risasi na mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji walioitikia mwito wa upinzani wa kuendelea na siku ya pili ya maandamano ya kupinga nia ya rais aliyeko madarakani Denis Sassou Nguesso kuwania muhula wake wa tatu. Waandamanaji wameweka vizuizi barabarani huku wakipigana na maafisa wa usalama. Maeneo ya Kusini mwa jiji hilo la Brazzaville ndio lililoathirika zaidi na makabiliano hayo baina ya waandamanaji na...
KITENGO cha upasuaji wa moyo Mhimbili, kimetangaza kujitenga kutoka kwenye kitengo na kuwa Taasisi inayojitegemea kwa lengo la kuboresha huduma zake na kuwa taasisi ya kisasa kwa Afrika Mashariki ikitatambulika kama Taasisi ya moyo ya JAKAYA KIKWETE. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam, wakati wa kutangaza mabadiliko hayo Kaimu mkuu wa taasisi hiyo Profesa MOHAMEDI JANABI amesema kuwa mbali na kujitenga huko pia taasisi hiyo imekuwa na mafaniko makubwa ambapo mwaka huu pekee 2015 wameweza kufanya upasuaji kwa...
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Mohamed Gharib Bilal leo amezindua rasmi Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano pamoja na kufungua Kituo cha kisasa cha kimataifa cha mawasiliano ya Intaneti kitakachojulikana kwa jina la IP-POP ikiwa ni jitihada za Serikali kuboresha na kuimarisha sekta ya TEHAMA nchini kwa kuboresha na kuongeza miundombinu itakayosaidia kutoa huduma bora katika Sekta ya mawasiliano. Akizungumza katika hafla hiyo Dokta Bilal amesema kuwa miundombinu hiyo ya mawasiliano ni muhimu kwa maendeleo...
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi MATHIAS CHIKAWE amewataka wananchi kutii sheria za nchi na zile za tume ya uchaguzi zinazoongoza uchaguzi mkuu sambamba na kufuata maelekezo yatakayotolewa na tume kabla na baada ya kupiga kura kwani kila mtanzania ana wajibu wa kuilinda amani kwa kufuata sheria za nchi bila kushurutishwa. Akizungumza na Efm Radio, leo jijini dar es salaam, waziri CHIKAWE amesema kuwa watanzania watambue baada ya uchaguzi mkuu maisha yanapaswa kuendelea kama kawaida hivyo itikadi za...
URUSI na Marekani zimetia saini makubaliano yanayotarajiwa kuzuia ndege za kijeshi za nchi hizo kushambuliana nchini Syria. Habari za kutiwa saini kwa mkataba huo zimethibitishwa na maafisa kutoka nchi zote mbili. Urusi ilianza kushambulia kwa ndege maeneo ya Syria Septemba 30, ikisema ilikuwa ikiwalenga wapiganaji wa kundi la Islamic State –IS, Nna wiki iliyopita, Marekani ilisema ndege za mataifa hayo zilikuwa zimeingia eneo moja la mapigano na zilikuwa karibu sana...