CCM KUHITIMISHA KAMPENI JANGWANI LEO

CCM KUHITIMISHA KAMPENI JANGWANI LEO

Like
228
0
Friday, 23 October 2015
Local News

CHAMA cha Mapinduzi CCM  leo kitafanya mkutano wake Mkubwa wa kuhitimisha kampeni zake kwa upande wa Mkoa wa Dar es salaam katika Viwanja vya Jangwani ambapo Mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho ataongea na wananchi wa mkoa huo kwa mara ya mwisho kuomba ridhaa yao ya kumpa kura siku ya Uchaguzi.

 

Kampeni za CCM zitafungwa Kitaifa kwa mikutano mikubwa ya kampeni katika mikoa saba  ambayo ni Mwanza, Tanga, Mbeya, Kigoma, Mtwara, Kilimanjaro na Mara ambapo Mikutano hiyo itaongozwa na viongozi wa CCM Kitaifa waliopo madarakani na wastaafu.

 

Hapo kesho,  Wagombea Ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao kwa namna mbalimbali.

Comments are closed.