CCM YAIBUKA KIDEDEA WILAYA YA KINONDONI

CCM YAIBUKA KIDEDEA WILAYA YA KINONDONI

Like
429
0
Tuesday, 16 December 2014
Local News

CHAMA CHA MAPINDUZI -CCM kimeibuka kidedea  katika Wilaya ya Kinondoni , baada ya kunyakua viti 132  kikifuatiwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA 34  na Chama Cha Wananchi-CUF 16.

Ofisa Uchaguzi wa Manispaa hiyo, VALENCE URASSA amesema Ccm imeshinda viti hivyo katika Mitaa 197 ya Wilaya hiyo huku Mitaa Miwili ikiwa haijafanya kabisa uchaguzi na 14 ikiharishwa.

Amebainisha kuwa Mitaa hiyo 14 inatarajiwa kufanya uchaguzi wake Disemba 21mwaka huu, na baadhi ya  taratibu za maandalizi zimeanza kukamilika.

Ameitaja baadhi ya Mitaa hiyo kuwa ni Mabibo, Mikocheni B, Ally Maua B, Mtaa wa Pwani , Tegeta,Kibwegere, Bwawani, Mtaa wa Mwinyi Mkuu, Mtambani na mingineyo.

Comments are closed.