CCM YAKAMILISHA UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE SINGIDA MASHARIKI NA KITETO

CCM YAKAMILISHA UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE SINGIDA MASHARIKI NA KITETO

Like
519
0
Tuesday, 18 August 2015
Local News

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi –CCM– Taifa katika kikao chake cha siku moja jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake Rais dokta Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto.

 

Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Ndugu Jonathan Njau –Singida Mashariki na Ndugu Emmanuel Papian John mgombea wa jimbo la Kiteto.

 

Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana.

Comments are closed.