CCM YAMPITISHA JOB NDUGAI KUGOMBEA USPIKA WA BUNGE

CCM YAMPITISHA JOB NDUGAI KUGOMBEA USPIKA WA BUNGE

Like
191
0
Monday, 16 November 2015
Local News

KAMATI ya Wabunge wote wa chama cha Mapinduzi-CCM-imempitisha Ndugu Job Ndugai kuwa mgombea wa Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia wagombea wenzake wa chama hicho kujitoa katika kinyang’anyiro hicho.

 

Akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa mgombea huyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa-CCM-Nape Nnauye amesema wana imani na Ndugai kuwa atashinda katika nafasi hiyo kutokana na uwezo wake wa kuongoza.

 

Kabla ya Ndugai kutangazwa kuwa ndiye atakayewania Uspika, wengine waliokuwepo katika kinyang’anyiro hicho ni pamoja na dokta Tulia Ackson na Abdulah Mwinyi.

Comments are closed.