CCM YATANGAZA KUKOMESHA MIGOGORO YA ARDHI

CCM YATANGAZA KUKOMESHA MIGOGORO YA ARDHI

Like
238
0
Wednesday, 02 September 2015
Local News

MGOMBEA  mwenza  wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu amesema Serikali itakayoundwa na chama hicho endapo itashika dola katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2015 itahakikisha inapima ardhi yote ya vijiji pamoja na kuainisha mipaka ili kukomesha migogoro ya ardhi.

 

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akinadi ilani ya CCM katika Majimbo mawili tofauti ya Kongwa na Chilonwa Mkoa wa Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kufanya kampeni kuwashawishi Watanzania waweze kukipa ridhaa tena Chama Cha Mapinduzi ili kiunde Serikali na kuwatumikia wananchi.

 

Kesho, Mgombea huyo mwenza wa nafasi ya urais kwa chama cha mapinduzi Samia Suluhu anatarajia kuanza mikutano ya hadhara katika jiji la Dar es Salaam na viunga vyake

IMG_0034

Comments are closed.