CCM YATIMUA WANACHAMA 25 BAADA YA KUKISALITI CHAMA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU

CCM YATIMUA WANACHAMA 25 BAADA YA KUKISALITI CHAMA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU

Like
309
0
Friday, 04 March 2016
Local News

CHAMA cha Mapinduzi-CCM-mkoa wa Kigoma kimewafukuza wanachama wake 25 baada ya kukisaliti chama wakati wa Uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 25 mwaka jana.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari, Katibu wa chama hicho mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala amesema kuwa uamuzi huo umetolewa katika kikao cha Halmashauri kuu ya Chama kilichofanyika machi 2 mwaka huu.

Naomi amesema baada ya kufanyika kwa Uchaguzi mkuu chama kilianza kufanya tathimini na changamoto walizokutana nazo wakati wa Uchaguzi na kugundua kuwa wanachama hao ni miongoni mwa waliosababisha.

Comments are closed.