CHADEMA KUFANYA MAANDAMANO KUMSINDIKIZA LOWASA KUCHUKUA FOMU

CHADEMA KUFANYA MAANDAMANO KUMSINDIKIZA LOWASA KUCHUKUA FOMU

Like
281
0
Monday, 10 August 2015
Local News

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimesema hakijapata taarifa ya Jeshi la polisi inayowazuia kufanya maandamano ya kumsindikiza mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi –UKAWA– Edward Lowasa anayetarajia kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo leo katika ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC- akiambatana na Mgombea mwenza Juma Duni Haji.

 

Jeshi la Polisi kanda  Maalumu ya Dar es salaam limepiga marufuku maandamano ya mgombea huyo kwenda kuchukua fomu NEC kwa maandamano yanayoanzia ofisi za CUF na badala yake yaanzie Chadema.

Akizungumza na wandishi wa habari jana, Mwenyekiti mwenza wa Umoja huo ambae pia ni mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia alisema tukio hilo linatarajia kufanyika kwa Maandamano makubwa ya amani yatakayoanzia Makao makuu ya Chama cha –CUF– Buguruni kuelekea ofisi za NEC ambapo baada ya kuchukua fomu Maandamano yataelekea Makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo –CHADEMA.

Comments are closed.