CHADEMA: NAFASI YOYOTE YA KUINDOA CCM LAZIMA ITUMIKE

CHADEMA: NAFASI YOYOTE YA KUINDOA CCM LAZIMA ITUMIKE

Like
194
0
Monday, 03 August 2015
Local News

CHAMA cha  Demokrasia na Maendeleo  CHADEMA kimesema nafasi yoyote ya kukiondoa Chama cha Mapinduzi CCM madarakani ni lazima itumike  kwa kutambua kuwa Chadema ni chama cha watu, na hivyo ni lazima waheshimu mawazo ya kila mtu mwenye lengo linalofanana na chama hicho.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam katika Mkutano wa baraza kuu la Chama cha Maendeleo na Demokrasia CHADEMA uliofanyika ili kupitia  na kuijadili ilani ya uchaguzi ambayo itapendekezwa katika mkutano mkuu kesho tarehe 4 Agosti 2015.

Akizungumza katika Mkutanohuo Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Freeman Mboye amesema ilikuwa lazima kama chama cha siasa kuweka mkakati wa kila wanayeweza kumpokea kutoka chama kingine ambacho sio mshirika wa UKAWA achukuliwe ili waweze kuunganisha Watanzania wote wenye mawazo chanya na nia ya dhati kwa Taifa.

Comments are closed.