CHADEMA YAITAKA SERIKALI KUONGEZA NGUVU KUPAMBANA NA AJALI

CHADEMA YAITAKA SERIKALI KUONGEZA NGUVU KUPAMBANA NA AJALI

Like
241
0
Wednesday, 15 April 2015
Local News

CHAMA cha Demokrasia na maendeleo -CHADEMA- Kimeitaka Serikali kuongeza nguvu ya Kupambana na Ajali za Barabarani kama ilivyo katika vita dhidi ya Mauaji ya Walemavu wa Ngozi kwani ajali zimekuwa na mchango mkubwa wa kumaliza nguvu kazi ya Taifa kila siku.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho kwa Upande wa Bara John Mnyika amesema badala ya Serikali kuwa ni sehemu ya kutuma salamu za rambirambi pindi ajali zinapotokea ni vyema serikali ikaeleza namna ambavyo imejipanga kupambana na ajali hizo.

Amesema hatua zilizoelezwa na kamanda wa usalama barabarani hazijitoshelezi kupambana na ajali hizo na kila siku Watanzania wanaendelea kupoteza maisha.

Comments are closed.