CHADEMA YAMTAKA RAIS KUWAWAJIBISHA WAHUSIKA WA SAKATA LA ESCROW

CHADEMA YAMTAKA RAIS KUWAWAJIBISHA WAHUSIKA WA SAKATA LA ESCROW

Like
301
0
Wednesday, 17 December 2014
Local News

KUFUATIA kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema, Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA- kimemtaka Rais JAKAYA KIKWETE kuwawajibisha haraka viongozi wengine waliohusika katika sakata la Akaunti ya TEGETA ESCROW.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Naibu katibu mkuu wa chama hicho JOHN MNYIKA amesema Rais alipaswa kumuwajibisha kabla hajachukuwa uamuzi huo wa kujiuzulu hivyo amemtaka kuchukua hatuwa za haraka kuwawajibisha watuhumiwa waliobaki akiwemo Waziri wa Nishati na Madini Profesa SOSPETER MUHONGO

 

Comments are closed.