CHAMA CHA PTF MASHUJAA CHAPATA USAJILI WA MUDA

CHAMA CHA PTF MASHUJAA CHAPATA USAJILI WA MUDA

Like
332
0
Monday, 09 November 2015
Local News

CHAMA cha Tanzania Patriotic Front-TPF-MASHUJAA kimepata usajili wa muda kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa wakati kikijiandaa kupata usajili wa kudumu kwa kuzingatia na kutimiza mashari na sheria ya usajili wa vyama vya siasa nchini.

 

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam baada ya usajili wa chama hicho Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa chama hicho kutambua kuwa chama ni kwa ajili ya wanachama na si kwa jili ya maslahi ya viongozi wa juu wanaokiongoza.

 

Naye Msajili Msaidizi wa Vyama vya siasa Sisty Nyahoza amewashauri viongozi wa TPF Mashujaa kuhakikisha wanatafuta wanachama halisi ili kuepuka changamoto mbalimbali zinazojitokeza ndani ya vyama zitakazoweza kusababisha chama kuvunjika na kukosa usajili wa kudumu.

Comments are closed.