CHENGE AISHAURI SERIKALI KUPUNGUZA VAT

CHENGE AISHAURI SERIKALI KUPUNGUZA VAT

Like
334
0
Tuesday, 25 November 2014
Local News

SERIKALI imeshauriwa kuangalia upya suala la marekebisho ya kodi katika baadhi ya vifungu vya sheria ikiwemo kupunguza kiwango cha –VAT– kutoka asilimia 18 hadi kufikia asilimia 16 hususani katika sekta ya utalii ili kuboresha uchumi wa nchi.

Ushauri huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya hesabu za bunge mheshimiwa ANDREW CHENGE wakati akitoa maoni ya kamati hiyo mara baada ya kusomwa kwa mara ya pili muswada waongezeko la thamani ya kodi nchini-VAT-la mwaka huu lililowasilishwa na waziri wa fedha mheshimiwa SAADA MKUYA.

Mbali na ushauri huo Mheshimiwa CHENGE ameiomba serikali pia kuondoa kabisa taratibu za utozaji kodi katika malighafi za kutengenezea dawa kwa kuwa dawa hazitozwi kodi.

 

Comments are closed.