Chicharito Apelekwa Real Madrid Kwa Mkopo

Chicharito Apelekwa Real Madrid Kwa Mkopo

Like
642
0
Monday, 01 September 2014
Slider

Chicharito

Huku dirisha la usajiri ulaya llikitarajiwa kufungwa usiku wa leo, tiimu ya Manchester United wamempeleka kwa mkopo Javie Hernandez “Chicharito kwenda timu ya Real Madrid  na wako mbioni kumwachia Danny Welbeck kwenda Tottenham au Everton.

Katika siku za hivi karibuni timu zote mbili yaani Manchester United na Real Madrid  zimeonyesha udhaifu katika safu ya ushambuliaji, ambapo  katika mechi dhidi ya Burnley Manchester United ilitoka suluhu huku Real Madrid ikichapwa jana usiku na Real Sociedad kwa mabao 3-1.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Mexico amekuwa hapati namba ya uhakika ya kudumu katika kikosi cha kwanza hata baada ya kocha mpya Mholanzi Louis Van Gaal kujiunga na timu hiyo mwezi uliopita.

Tayari mchezaji Chicharito ametambulishwa rasmi hii leo na bado haijaeleweka dili la mchezaji huyo kuhamia Real Madrid ilikuwa ni sehemu ya makubaliano ya uhamisho wa mchezaji wa kimataifa wa Argentina Angel Di Maria.  Duru nyingine zikiarifu kuwa kulikuwa na mpango wa chini chini ambao ulikuwa umhusishe Falcao kwenda Real Madrid lakini baada ya mazungumzo Falcao amekwenda Manchester United na Chicharito kuhamia Real.

Comments are closed.