CHIEF YEMBA ATANGAZA KUWANIA KITI CHA USPIKA WA BUNGE

CHIEF YEMBA ATANGAZA KUWANIA KITI CHA USPIKA WA BUNGE

Like
411
0
Monday, 16 November 2015
Local News

ALIYEKUWA mgombea urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ADC, Chief Lutayosa Yemba, ametangaza kugombea kiti cha Uspika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.

 

Chief Yemba, ameyasema hayo jijini Arusha, alipokuwa akitoa Tathimini yake kwa vyombo vya habari kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu, pamoja na tathimini ya uchaguzi wa nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha ambao unatarajiwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu.

 

Amesema baada ya kuanguka kwenye urais, sasa anaelekeza nguvu zake kwenye Usipika, ambako ana uhakika wa kushinda kwa kuwa ana sifa na vigezo  vinavyotakiwa.

Comments are closed.