CHINA KUFUNGA DARAJA LA VIOO BAADA YA WIKI MBILI

CHINA KUFUNGA DARAJA LA VIOO BAADA YA WIKI MBILI

Like
539
0
Monday, 05 September 2016
Slider

Daraja la vioo lililojengwa juu nchini Uchina ililosifiwa kwa kuvunja rekodi lilipozinduliwa siku 13 tu zilizopita limefungwa.

maafisa wanasema serikali inapanga kufanya ukarabati wa dharura wa eneo hilo na hivyo kufunga daraja hilo Ijumaa, ambapo tarehe ya kufunguliwa tena itatangazwa

Lakini Kituo cha televisheni cha Marekani CNN kimesema kuwa msemaji amewaambia kuwa daaja hilo linaloelea juu “limekuwa likitembelewa na wageni wengi kupita uwezo wake “.

Amesema kuwa hakuna ajali iliyowahi kutokea na daraja halikuwa na ufa wala mpasuko wowote.

Daraja hilo lenye urefu wa mita 430, ambalo ujenzi wake uligarimu $3.4 milioni, linaunganisha mabonde mawili ya milima ya Zhangjiajie, katika jimbo la Hunan.

Daraja hilo Linaeloelea umbali wa mita 300 kutoka kwenye bonde linasemekana kuwavutia sana waandaaji wa filam.

Lilipofunguliwa lilisemekana kuwa daraja refu zaidi kwa kimo na upana zaidi lililotengenezwa kwa vioo duniani.

screenshot of Weibo post with Chinese characters

Daraja hilo linaweza kuwapokewa wageni 8,000 kwa siku , lakini msemaji ameiambia CNN kwamba mara 10 ya watu hao walitaka kulizulu kila siku.

Akijibu kuhusu tangazo hilo, mmoja wa watumiaji wa mitandao ya kijamii aliandika : “Nimelipa kila kitu na sasa mnasema mnafunga…Mnanitania?”

Comments are closed.