Uchina inasema kuwa itaanza kuwatembeza kwa meli raia wanaotaka kuzuru visiwa vinavyozozaniwa vilivyoko kusini mwa bahari ya China.
Vyombo vya habari vya serikali vinasema kuwa miaka minne ijayo, ziara hizo zitakuwa zikitoka kisiwa cha Hainan kabla ya kuelekea katika kisiwa chengine cha Nansha na kisha Spratley.
Mapema juma hili, kampuni kubwa ya meli, Cosco, ilitangaza kuwa itaanzisha ziara za meli katika visiwa vingine vilivyoko katika eneo la kusini mwa bahari ya China, Paracels.
Kutokana na shughuli kadhaa za kijeshi na safari za kiraia katika eneo hilo, Uchina imeanza juhudi zinazoonekana kuonyesha kuwa inataka kuthibiti utawala wa eneo hilo linalozozaniwa.