CHINA YAIKOSOA MAREKANI JUU YA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA UDUKUZI

CHINA YAIKOSOA MAREKANI JUU YA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA UDUKUZI

Like
301
0
Friday, 05 June 2015
Global News

CHINA imeitaja Marekani kuwa imekosa kuwajibika kwa kudai kuwa wadukuzi wa china ndio waliosababisha udukuzi wa taarifa za ofisi ya serikali ya Marekani.

Wizara ya mambo ya nje ya china imesema ni vigumu kujua chanzo cha udukuzi huo na kwamba dhana isiyo na ushahidi wowote wa kisayansi haitasaidia.

Shirika la ujasusi la –FBI- nchini Marekani linachunguza namna wadukuzi wa komputa walivyoweza kuingilia taarifa hizo binafsi za wafanyakazi wa serikali wapatao milioni nne .

Comments are closed.