CHINA YAPIGA MARUFUKU UVUTAJI WA SIGARA KATIKA MAENEO YA WAZI

CHINA YAPIGA MARUFUKU UVUTAJI WA SIGARA KATIKA MAENEO YA WAZI

Like
165
0
Monday, 01 June 2015
Global News

SERIKALI ya China imepiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo yote ya wazi katika mji wa Beijing.

Maelfu ya maafisa wameanza kufanya ukaguzi katika maeneo yote yaliyoanishwa kutohusika na kitendo cha uvutaji sigara ambapo kwa wale watakaokiuka kufuata sheria hiyo watapigwa faini.

Hata hivyo tafiti zinasema kuwa  China ina jumla ya wavutaji sigara milioni 300 wakati sheria ya kusitisha uvutaji sigara katika maeneo ya wazi ya mji wa Beijing ilipopitishwa kwa mara ya kwanza na kushindwa kutekelezeka.

Comments are closed.