CIA YADAI KUIVURUGA AL QAEDA

CIA YADAI KUIVURUGA AL QAEDA

Like
230
0
Monday, 02 May 2016
Global News

MKURUGENZI wa CIA John Brennan amesema kwa miaka mitano iliyopita Marekani imeharibu kwa kiasi kikubwa kundi la Al Qaed baada ya kuuawa kwa kiongozi wake mkuu Osama bin Laden kutokana na uvamizi wa vikosi maalum nchini Pakistan.

Brennan amesema kuwa Bin Laden alikuwa nembo na mwenye mikakati imara na muhimu na ilikuwa lazima kumuondoa mtu huyo ambaye amehusika katika mashambulizi ya kigaidi mjini Washington na New York Septemba 11.

Mkuu huyo wa CIA ameongeza kuwa kumuondoa kiongozi wa IS Abu Bakr Al-Baghdadi inaweza kuwa na athari kubwa kwa mataifa mbalimbali.

Comments are closed.