CIA YATETEA MBINU ZAKE ZA KIKATILI KUWAHOJI WATUHUMIWA WA UGAIDI

CIA YATETEA MBINU ZAKE ZA KIKATILI KUWAHOJI WATUHUMIWA WA UGAIDI

Like
326
0
Friday, 12 December 2014
Global News

MKURUGENZI wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA, JOHN BRENNAN, kwa mara nyingine ametetea matumizi ya mbinu za kikatili wakati wa kuwahoji watuhumiwa wa ugaidi baada ya shambulio la Septemba 11 nchini Marekani.

BRENNAN amekiri kuwa baadhi ya mbinu zilizotumika zilikuwa za kuchukiza. Lakini amesisitiza kuwa baadhi ya wafungwa ambao walipitia mbinu hizo, ambazo zilikuwa ni pamoja na kuwazamisha kwenye maji, kuwafadhaisha na kuwanyima usingizi zimesaidia kuokoa maisha ya Wamarekani na zilisaidia kumpata OSAMA BIN LADEN.

Amejibu ripoti ya Kamati ya Upelelezi ya Baraza la Senate la Marekani, ripoti ambayo imekosoa vikali mbinu za mahojiano za CIA, ambazo zinasemekena zimekuwa za mateso kwa watuhumiwa.

141210082909_cia_ukatili_512x288_bbc_nocredit us

 

 

Comments are closed.