CLASICO ZA UHISPANIA KUTIMUA VUMBI NOVEMBA, APRIL

CLASICO ZA UHISPANIA KUTIMUA VUMBI NOVEMBA, APRIL

Like
306
0
Thursday, 16 July 2015
Slider

Ligi mpya ya kabumbu itang’oa nanga wikendi ya Agosti 23, na mechi kali za “clasico” kati ya Real Madrid na Barcelona zitachezwa Novemba na Aprili, shirikisho la soka nchini humo lilisema Jumanne.

Mechi hizo kati ya mahasimu hao wa jadi zitachezwa Novemba 8 mjini Madrid na Aprili 3 mjini Barcelona, Shirikisho la Soka la Uhispania lilisema baada ya droo kufanywa makao makuu ya shirikisho hilo.

Mabingwa wa ligi Barcelona watakuwa wakipigania kuhifadhi mataji ya Ligi ya Uhispania, Kikombe cha Ligi na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya waliyoshinda msimu uliopita.

Wana mwanzo wenye shughuli nyingi kwa msimu wao mpya wakianza kwa mechi za nyumbani na ugenini dhidi ya Athletic Bilbao Agosti 14 na 21 katika Super Cup ya Uhispania.

Taji hilo hukutanisha washindi wa ligi na washindi wa Copa del Rey – au, kama inavyofanyika sasa, klabu inayomaliza ya pili, kwani Barca pia walishinda kikombe hicho.

Barca na Athletic watakutana tena siku chache baadaye, wakicheza mechi yao ya kwanza ligini Bilbao wikendi ya Agosti 22-23.

Real Madrid, waliomaliza wa pili ligini msimu uliopita, watacheza mechi yao ya kwanza dhidi ya vijana wapya ligini Sporting Gijon.

Atletico Madrid walio maliza wa tatu nao watakutana Las Palmas, waliopandishwa daraja majuzi.

Mechi za mwisho ligini zitachezwa Mei 15.

Comments are closed.