CLINTON NA SANDERS WACHUANA VIKALI FLORIDA

CLINTON NA SANDERS WACHUANA VIKALI FLORIDA

Like
231
0
Thursday, 10 March 2016
Global News

WAGOMBEA wa urais kupitia chama cha Demokrat nchini Marekani Hillary Clinton na mwenzake Bernie Sanders wamekabiliana vikali kuhusu swala la uhamiaji pamoja na maswala mengine katika mjadala mjini Florida.

Mjadala huo uliokuwa moja kwa moja kupitia runinga mjini Miami ulifanyika siku chache tu kabla ya uteuzi wa jimbo la Florida.

Huku wajumbe 246 wakiwa watapiganiwa na vigogo hao wawili wa chama cha Demokrat jimbo hilo la Kusini linaelezwa kuwa ni muhimu sana.

Comments are closed.