CONGO BRAZZAVILLE: POLISI WATUMIA RISASI NA MABOMU YA MACHOZI KUTAWANYA WAANDAMANAJI

CONGO BRAZZAVILLE: POLISI WATUMIA RISASI NA MABOMU YA MACHOZI KUTAWANYA WAANDAMANAJI

Like
229
0
Wednesday, 21 October 2015
Global News

POLISI nchini Congo Brazaville wamefyatua risasi na mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji walioitikia mwito wa upinzani wa kuendelea na siku ya pili ya maandamano ya kupinga nia ya rais aliyeko madarakani Denis Sassou Nguesso kuwania muhula wake wa tatu.

 

Waandamanaji wameweka vizuizi barabarani huku wakipigana na maafisa wa usalama.

 

Maeneo ya Kusini mwa jiji hilo la Brazzaville ndio lililoathirika zaidi na makabiliano hayo baina ya waandamanaji na polisi.

Comments are closed.