CONGO: UPINZANI WATISHIA MAANDAMANO

CONGO: UPINZANI WATISHIA MAANDAMANO

Like
211
0
Tuesday, 15 September 2015
Global News

VYAMA kadhaa vya upinzani nchini Congo vimeitisha maandamano katika mji mkuu wa Taifa hilo Kinshasa juu ya kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu wa Urais uliotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka 2016.

Wiki iliopita mahakama ya kikatiba nchini humo ilitaka siku ya uchaguzi huo kutangazwa upya hatua ambayo wapinzani wamesema ni ya kutaka rais Joseph Kabila kusalia madarakani zaidi hata baada ya kukamilika kwa muda wake uliowekwa kikatiba.

Rais Joseph Kabila amekuwa madarakani tangu baba ake aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo auwawe mwaka 2001.

Comments are closed.