CONTE ANG’AKA CHELSEA KUPIGWA 3-0 NA BARCELONA

CONTE ANG’AKA CHELSEA KUPIGWA 3-0 NA BARCELONA

Like
394
0
Thursday, 15 March 2018
Sports

Antonio Conte greets Lionel Messi at the final whistle.

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema alihisi kwamba kichapo cha 3-0 ambacho klabu yake ilipokezwa katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano “hakikuwa cha haki”.

Lionel Messi alifunga mabao mawili naye Ousmane Dembele akafunga moja – bao lake la kwanza akichezea Barca – na kuwasaidia miamba hao wa Uhispania kuondoka na ushindi wa jumla wa 4-1.

Mechi ya kwanza uwanjani Old Trafford ilikuwa imemalizika 1-1.

Matokeo hayo yaliwaondoa Chelsea kutoka kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu na msimu ujao wanakabiliwa na kibarua cha kufuzu kutokana na ushindani mkali kwenye nafasi nne za kwanza Ligi ya Premia.

“Hatuna majuto,” alisema Conte.

“Ukiitazama mechi hiyo, utaona kwamba matokeo hayo hayakuwa ya haki.”

Conte alikiri kwamba Messi – aliyefunga pia bao la Barca mechi ya kwanza Stamford Bridge – ndiye aliyekuwa mwamuzi wa nani mbabe kati ya timu hizo mbili.

Bao la pili la mshambuliaji huyo wa Argentina uwanjani Nou Camp lilifikisha 100, idadi ya mabao ambayo ameyafunga Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Mpinzani wake mkuu kutoka Real Madrid Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi akiwa na mabao 117.

Hata hivyo, Messi amefikisha idadi hiyo akiwa amecheza mechi 14 chini ya alizocheza Ronaldo ndipo afikishe mabao hayo.

“Tunazungumzia mchezaji bora zaidi duniani,” alisema Conte.

“Huwa anafunga mabao 60 kila msimu – ni mchezaji mzuri ajabu. Barcelona walikuwa na ufasaha sana wakishambulia.”

Comments are closed.