COUNTINHO AITOA LIVERPOOL KIMASOMASO

COUNTINHO AITOA LIVERPOOL KIMASOMASO

Like
353
0
Monday, 10 August 2015
Slider

Bao la kiuchawi kutoka mganga wa kutoka Brazil, Phillipe Coutinho, lilianzisha kampeni ya musimu huu ya Liverpool kwa ushindi walipolipisha kisasi dhidi ya Stoke City kwa kuwanyuka vijana wa nyumbani 1-0 Jumapili.

Liverpool walirudi uwanja wa Britannia ambapo waliandaliwa kichapo kikali cha 6-1 katika ngoma ya kufunga muhula uliopita lakini waliweza kuibuka na ushindani uliotafutwa kwa hima katika mechi ambayo ilibanwa kiubunifu.

Hakuna kipa alifanyishwa kazi ya kuokoa lango lake katika makabiliano yalioonekana kufikia tamati kwa sare nunge huku washambuliaji wa pande zote mbili wakikosa mbinu ya kupenya miamba iliyokuwa mbele yao.

Ikisalia dakika nne muda wa kawaida kuisha, Coutinho, mmoja wa wachezaji watano wa kikosi cha kwanza walionusurika kutoka aibu ya Mei waliweza kuwapatia Liverpool alama zote tatu kwa njia spesheli.

Meneja Brendan Rodgers ambaye alikuwa tayari ameashiria nyota huyo aondoke uwanjani na mshambuliaji mpya Danny Ings apate nafasi ya kwanza na Liverpool aliungana na wengine ugani huo kubaki vinywa wazi wakati kiungo hicho shambulizi alimiliki mpira kutoka kimo na kuwachilia mzinga mkali ambao ulifyatuka hadi nyavuni za Stoke bila pingamizi.

Comments are closed.