MFUKO wa Watoto wa Umoja wa mataifa UNICEF imeadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa mkataba wa haki za mtoto CRC na taasisi mbalimbali nchini kwa kutambua haki za Watoto wa Tanzania.
Hafla hiyo iliyobeba kauli mbiu ya “Watoto milioni 23: Tuongee kuhusu haki zao” imehusisha majadiliano ya namna ya kulinda na kuboresha sheria na haki za watoto na umuhimu wake.
Akizungumza katika hafla hiyo Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto PINDI HAZARA CHANA, amesema mtoto anatakiwa kutunzwa, kulindwa, kutobaguliwa na kuendelezwa na sio kuajiriwa au kuwa ombaomba.