CRICKET: RICHIE BENAUD AFARIKI DUNIA

CRICKET: RICHIE BENAUD AFARIKI DUNIA

Like
264
0
Friday, 10 April 2015
Slider

Aliekuwa nahodha wa timu ya cricket ya Australia Richie Benaud amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84.

Benaud alistaafu mchezo huo mwaka 1964 na kuingia kwenye taaluma ya habari ambapo kazi yake ya mwisho kama mchambuzi aliifanya nchini Uingereza mwaka 2005 kwenye michuano ya Ashes Series na baadae alikwenda kukitumikia kituo cha Channel Nine huko Australia mpaka mwaka 2013.

Mwezi November aligundulika kuwa na ugonjwa wa saratani ya ngozi

Kufuatia heshima aliyojiwekea kwenye mchezo huo duniani wadau mbalimbali wametoa salamu za rambirambi na kumuelezea marehemu jinsi wanavyomfahamu lakini pia mwenyekiti wa mchezo wa cricket nchini Australia amesema seriakali kwakutambua mchango wa mkongwe huyo imetangaza siku ya maombolezo kitaifa

Comments are closed.