CRIS BROWN AMTAKA MAMA WA MTOTO WAKE AHAMIE L.A

CRIS BROWN AMTAKA MAMA WA MTOTO WAKE AHAMIE L.A

Like
318
0
Wednesday, 25 March 2015
Entertanment

Kwa kawaida ya mastar wengi huko Hollywood huwakimbia waschana wanaowapa mimba pasi na matarajio yao zaidi inapotokea kwa michepuko yao ila hii ni tofauti kwa star aliemaliza kutumikia kifungo cha nje alipokutwa na hatia za kumtandika aliekuwa mpenzi wake Rihanna hapa namzungumzia Cris Brown

Hivi karibuni kumekuwa na stori za star huyo kuvunja mahusiano yake na mwanadada karrueche tran kufuatia kugundulika kuwa na mtoto aliezaa na mschana mwingine.

Cris Brown amekuwa karibu na Nia Guzman toka iliporipotiwa kuwa yeye ni baba wa mtoto mwenye miezi tisa na amekuwa akijivunia nafasi hiyo ya kuwa baba wa mtoto huyo richa yakukutana na kikwazo cha umbali kutoka eneo analoishi Cris na lile analoishi mwanae.

Chanzo cha karibu na msanii huyu kinaeleza kuwa Cris amemuomba Nia kwenda kuishi Los angels na yupo tayari kulipia gharama za maisha kwa kulipa kodi ya nyumba iwapo ofa yake itakubaliwa

Imeelezwa kuwa kwa sasa hana mahusiano ya kimapenzi na mschana huyo bali anahitaji kuwa na mahusiano karibu na mwanae. Pia ameongeza anapenda kumuona kila siku

Kwa sasa Cris na Nia wapo kwenye hatua za mwanzo za makubaliano juu ya matunzo ya mtoto huyo na inaelezwa kuwa kiasi cha malipo anayolipia kwenye huduma za mtoto huyo ni kikubwa kuliko kiwango anachohitajika kulipa suala hilo litakapofikishwa mahakamani

 

Comments are closed.