CUF YAGOMA KURUDIA UCHAGUZI ZANZIBAR

CUF YAGOMA KURUDIA UCHAGUZI ZANZIBAR

Like
269
0
Monday, 11 January 2016
Local News

WAKATI kesho ni maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi, Chama cha Wananchi –CUF, kimesema hakitakubali marudio ya uchaguzi wa urais visiwani Zanzibar.

Taarifa ya chama hicho ambayo imesomwa leo na aliyekuwa mgombea wa urais wa CUF katika uchaguzi wa 25 Oktoba mwaka jana,  Maalim Seif  imeeleza kuwa hakuna hoja wala msingi wa kikatiba na kisheria wa uchaguzi  huo kurudiwa.

Taarifa hiyo imeonyesha kutoa mapendekezo ya kuondolewa kwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha.

Comments are closed.