CUF YAMTAKA RAIS KUWAWAJIBISHA PINDA NA GHASIA

CUF YAMTAKA RAIS KUWAWAJIBISHA PINDA NA GHASIA

Like
270
0
Tuesday, 16 December 2014
Local News

CHAMA cha Wananchi CUF kimemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kuwawajibisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda Pamoja na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI Hawa Ghasia kwa kile wanachokidai kushindwa kusimamia Vizuri Chaguzi za serikali za Mitaa.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuwa kumekuwa na malalamiko na mapungufu mengi katika chaguzi hizo zilizosababishwa na utendaji mmbovu wa usimamizi.

Aidha amesema kuwa Rais anapaswa kuhakikisha kuwa mchakato wa Daftari la kudumu la wapiga kura unaendeshwa vizuri ili uchaguzi ufanyike kwa amani bila kasoro kama zilizojitokeza sasa.

 

 

Comments are closed.