CUF YASHUKIA MFUMO WA BVR

CUF YASHUKIA MFUMO WA BVR

Like
319
0
Thursday, 26 March 2015
Local News

CHAMA cha wananchi- CUF kimesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kutumika kwa daftari la kudumu la wapiga kura lililoandikishwa mwaka 2010 kutokana na mapungufu yaliyopo katika mfumo mpya wa uandikishaji wa sasa wa BVR.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo katika ofisi za chama hicho buguruni jijini Dar es salaam, Naibu mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho Abdul Kambaya amesema kuwa hadi sasa serikali haijafikia lengo la uandikishaji walilojiwekea.

Amesema kutokana na hali hiyo na msisitizo wa zoezi hilo kuisha April 30 kuna uwezekano wa kutumika daftari la zamani ambalo Serikali ilikiri kuwa na mapungufu makubwa.

Comments are closed.