CUF YATARAJIA KUMTANGAZA MAHARAGANDE KUGOMBEA NAFASI YA UBUNGE MOROGORO MJINI

CUF YATARAJIA KUMTANGAZA MAHARAGANDE KUGOMBEA NAFASI YA UBUNGE MOROGORO MJINI

Like
405
0
Tuesday, 31 March 2015
Local News

KUELEKEA Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, imeelezwa kuwa Chama  cha Wananchi CUF kinachounda Umoja wa Katiba wa wananchi –UKAWA, kinatarajia kumsimamisha MBARARA MAHARAGANDE kuwa Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Morogoro mjini.

Akizungumza na Kituo hiki MAHARAGANDE amesema kuwa anauhakika wa kushinda nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba  mwaka huu kwa kile alichodai kuwa wananchi wa Morogoro wamepania kufanya mabadiliko.

Amesema kuwa wananchi wamechoshwa na ahadi zisizotekelezeka huku hali ya maisha ikiwa duni na kukabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za miundo mbinu.

Comments are closed.