DANNY WELBECK AIONDOA MAN U KOMBE LA FA

DANNY WELBECK AIONDOA MAN U KOMBE LA FA

Like
259
0
Tuesday, 10 March 2015
Slider

Danny Welbeck amerejea katika viwanja vya old Trafford kwenye mechi iliyochezwa jana ambapo timu ya Arsenal imeibuka na ushindi wa 2-1 baada ya kuichapa Manchester united kwenye uwanja wa nyumbani

Mshambuliaji wa Uingereza Welbeck aliejiunga na klabu ya Arsenal akitokea Man u alishinda goli lililoipa Arsenal ushindi wao wa kwanza katika viwanja hivyo tangu mwaka 2006

Goli la kwanza la Arsenal lilifungwa na Nacho Monreal katika kipindi cha kwanza cha mchezo huolakini baadae Wayne Rooney alisawazisha bao hilo

Goli hilo la Danny Welbeck ndilo goli lililoiondoa klabu yake hiyo ya zamani kwenye michuano ya FA usiku wa jana

Moja kati ya matukio yaliyowashangza wengi hapo jana ni furaha ya mchezaji huyo baada ya kushinda bao hilo ambapo kwa kawaida wachezaji wengi wanapokutana na timu walizokuwa wakichezea wanapataga wakati mgumu kushangilia magoli

_81531480_mon-epa _81531483_roo-epa _81531485_wel-ap _81531588_danny-getty _81531589_di-reuters

Comments are closed.