DAVID GINOLA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS FIFA

DAVID GINOLA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS FIFA

Like
326
0
Friday, 16 January 2015
Slider

Mchezaji wa zamani wa Ufaransa David Ginola amesema kuwa atasimama dhidi ya Sepp Blatter kuwania Urais wa shirikisho la kandanda duniani,Fifa.

Lakini richa ya kuwa imetangazwa hivyo hakuna uhakika kama Ginola ataendelea na nia yake.

Hali hii inakuja kwakuzingatia vigezo ambapo mgombea anahitajika kuungwa mkono na vyama vitano vya soka na kigezo kingine anapaswa kuwa amejihusisha na soka kwa miaka miwili kati ya mitano iliyopita

Mchezaji huyo mwenye miaka 47 , aliichezea Ufaransa, pia club ya nchi hiyo Paris St Germain kabla ya kujiunga na New Castle United kwa kitita cha Pauni milioni 2.5 mwaka 1995.

Zoezi la Uteuzi wa nafasi ya urais wa fifa litafungwa tarehe 29 mwezi huu.Blatter amekuwa Rais wa Fifa tangu mwaka 1998 anawania muhula wa tano sasa.

Comments are closed.