DAWA ZA KULEVYA ZACHAFUA HALI YA HEWA MEXCO

DAWA ZA KULEVYA ZACHAFUA HALI YA HEWA MEXCO

Like
158
0
Tuesday, 14 July 2015
Global News

WAZIRI wa mambo ya ndani wa Mexco ameitisha mkutano wa magavana wa majimbo ili kujadili namna ya kuepusha vurugu zinazoweza kutokea kufuatia kutoroka kwa mtuhumiwa maarufu wa biashara ya dawa za kulevya.

Vyombo vya usalama ndani ya Mexico na maeneo ya jirani kwa sasa vinamtafuta Joaquin Guzman ambaye ni mfanyabiashara mkubwa wa dawa hizo kwa kutoroka katika mazingira yanayodaiwa kuwa ni ya rushwa.

Naye Rais wa Mexco Enrique Pena Nieto amesema kuwa ana Imani kuwa idara za usalama zitamkamata mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuwa mhimili mkubwa duniani kwa biashara hiyo na ambaye alitoroka kutoka katikati ya ulinzi mkali.

Comments are closed.