DAWA ZA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VVU ZASAIDIA WATOTO KUZALIWA SALAMA

DAWA ZA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VVU ZASAIDIA WATOTO KUZALIWA SALAMA

Like
305
0
Tuesday, 17 February 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa Kuimarika kwa upatikanaji wa huduma ya kupewa dawa za kuzuia maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa akina mama wajawazito ili kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kumesababisha watoto wengi kuzaliwa wakiwa salama.

Hayo yamesema na Dokta Zulfa Msami wakati akisoma taarifa ya kituo cha Afya cha Manispaa ya Lindi kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete alipotembelea kituo hicho.

Dokta Msami amesema kwa mwaka 2014 akina mama wajawazito 241 kati ya 280 walipima VVU katika kituo hicho kati yao 30 sawa na asilimia 12 walikutwa na maambukizi na kwa upande wa watoto ambao mama zao walikuwa na maambukizi 35 walipimwa na mtoto mmoja aligundulika kuwa na maambukizi.

Comments are closed.