DAWASCO YATAKIWA KUWEKA MITA ZA KIELEKTRONIKI

DAWASCO YATAKIWA KUWEKA MITA ZA KIELEKTRONIKI

1
679
0
Thursday, 05 July 2018
Local News
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) wakati wa ziara ya kujitambulisha mapema leo ofisi za DAWASCO. Picha zote na Cathbert Kajuna – Kajunason/MMG.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja alitoa maelekezo machache wakati wa ziara ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa ofisi za DAWASCO mapema leo alipofanya ziara ya kujitambulisha.
Wafanyakazi wa DAWASCO wakifuatilia maelezo ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akipokelewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati akipokelewa ofisi za DAWASCO mapema leo alipofanya ziara ya kujitambulisha.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akiagana na wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) wakati wa ziara ya kujitambulisha mapema leo ofisi za DAWASCO.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Makame Mbarawa. 
Waziri wa Maji na umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa ameliagiza Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASCO) kuhakikisha linabadili mfumo wa mita zinazotumika sasa kuhamia kwenye mfumo wa kieletroniki ambao utawafanya wateja wake walipe kabla ya kutumia hatua ambayo itasaidia katika ukusanyaji wa mapato na kudhibiti upotevu wa mapato.
Maagizo hayo ameyatoa mapema leo Julai 4, 2018 alipotembelea shirika hilo mara baada ya kuteuliwa mwishoni mwa wiki kuingia kwenye wizara ambapo amesema awali aliwahi kuteuliwa lakini alikaa muda mfupi ambapo aliacha maagizo kadhaa ikiwemo hilo la mita ambalo kwa sasa amewataka walitilie mkazo.
Amesema kuwa malengo ya wizara yake kuwa ni kuwafikishia wananchi wanyonge huduma ambayo ni muhimu na hivyo amewataka watendaji wa DAWASCO kutoka na kwenda kushughulikia kero za wananchi na kuhakikisha zinatatuliwa kwa wakati. “Nawaomba tufanye kazi kwa uadilifu na kuacha kuwanyanyasa wananchi kwa kuwapelekea bili zisizoeleweka kabisa maana hizi mita za zamani zinapoteza maji na vile vile fedha ya shirika,”
Amesema Prof. Mbarawa. Aidha ameongeza suala la wafanyakazi kuingia mikataba ya kiutendaji ambayo anaamini endapo itafuatwa itaweza kubadilisha sura ya shirika hilo huku akiigiza bodi ya wakurugenzi kuhakikisha inaongeza wateja kutoka 290,000 waliopo sasa hadi kufikia 850,000 kwa mwaka hatua ambayo itaongeza mapato zaidi ya mara tatu lakini pia amesema suala la upotevu wa maji lipewe kipaumbele ili kudhibiti fedha nyingi zinazopotea kupitia upotevu huo.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kwa sasa DAWASCO ina mipango mingi ambayo inakwenda kutekelezwa na ndiyo maana ameamua kuingia mikataba na watumishi wa shirika hilo ili kufikai malengo hayo kwa urahisi huku likiendelea kubuni mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamaoto zinazojitokeza ikiwemo upotevu wa maji ambapo mita 155 zitabadilishwa ambazo zilikuwa chakavu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *